top of page

Sababu Tano za Kutokuwa na hofu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Mar 31
  • 2 min read
ree

“Msiogope, enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi ufalme.” (Luka 12:32)

 

Sababu ambayo Mungu anataka tusiogope kuhusu pesa au vitu vingine vya ulimwengu ni kwa sababu kutoogopa huko - uhuru huo kutoka wasiwasi - utakuza mambo makuu matano juu yake.

 

Kwanza, kutoogopa kunaonyesha kwamba tunamthamini Mungu kama Mchungaji wetu. “Msiogope, enyi kundi dogo.” Sisi ni kundi lake na yeye ni Mchungaji wetu. Na ikiwa yeye ndiye Mchungaji wetu, basi Zaburi 23:1 inatumika: “Bwana ndiye Mchungaji wangu; Sitapungukiwa na kitu” - yaani, sitapungukiwa na chochote ninachohitaji kikweli.

 

Pili, kutoogopa kunaonyesha kwamba tunamthamini Mungu kama Baba yetu. “Baba yenu ameona vyema kuwapa Ufalme.” Sisi si kundi lake dogo tu; sisi ni watoto wake pia, naye ni Baba yetu. Anajali sana na anajua unachohitaji na atakufanyia kazi uwe na uhakika kwamba una kile unachohitaji.

 

Tatu, kutokuwa na wasiwasi kunaonyesha kwamba tunamthamini Mungu kama Mfalme. “Msiogope, enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa Ufalme .” Anaweza kutupa “Ufalme” kwa sababu yeye ndiye Mfalme. Hii inaongeza kipengele kikubwa cha nguvu kwa yule amnbaye hutupatia sisi. "Mchungaji" inamaanisha ulinzi na utoaji. “Baba” humaanisha upendo na huruma na mamlaka na utoaji na mwongozo. “Mfalme” humaanisha nguvu na enzi kuu na utajiri.

 

Nne, kutoogopa kunaonyesha jinsi Mungu alivyo huru na mkarimu. Zingatia, yeye anatupa Ufalme. “Msiogope, enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa Ufalme.” Hauzi ufalme, hakodishi ufalme, wala hakopeshi ufalme. Utajiri hauna kikomo hana hitaji la malipo yetu. Kwa hivyo, Mungu ni mkarimu na huru kwa fadhila zake. Na hivi ndivyo tunavyomtukuza juu yake wakati ambao hatuogopi, lakini tumwamini kwa mahitaji yetu.

 

Hatimaye, kutoogopa—kutokuwa na wasiwasi—kunaonyesha kwamba tunaamini kwamba kweli Mungu anataka kufanya hivi. “Msiogope, enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema Ufalme.” Inamfurahisha. Hana kinyongo. Inamfanya afurahi kutupa Ufalme. Sio sisi sote tulikuwa na baba kama hawa, ambao walifurahishwa kwa kutoa badala ya kupata. Lakini huzuni hiyo sio jambo kuu tena, kwa sababu sasa unaweza kuwa na huyo Baba, na Mchungaji, na Mfalme.

 

Kwa hiyo, lengo la mstari huu ni kwamba tunapaswa kumthamini Mungu kama Mchungaji wetu, Baba yetu, na Mfalme wetu ambaye ni mkarimu na mwenye furaha kutupa ufalme wa Mungu — kutupa mbingu, kutupa uzima wa milele na furaha, na kila kitu tunachohitaji kufika huko.

 

Tukimuona Mungu ni wa thamani kwa namna hii, hatutakuwa na hofu na Mungu ataabudiwa.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page