top of page

Salama Kadri Mungu Alivyo Mwaminifu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 1 min read

ree

Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza. (Warumi 8:30)


Kati ya umilele uliopita katika uteuzi wa Mungu tangu zamani, na wakati ujao wa umilele katika utukufu wa Mungu, hakuna hata mmoja aliyepotea.


Hakuna anayekusudiwa kuwa mwana ambaye hatapokea mwito. Na hakuna aliyeitwa anayeshindwa kuhesabiwa haki. Na hakuna mtu anayehesabiwa haki asiyeweza kutukuzwa. Huu ni mnyororo wa chuma usioweza kukatika wa uaminifu wa agano la kimungu.


Na hivyo Paulo anasema, 


Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Kristo Yesu. (Wafilipi 1:6)


[Yeye] Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Yesu Kristo, Bwana wetu ni mwaminifu. (1 Wakorintho 1:8-9)


Hizi ni ahadi za Mungu wetu asiyeweza kusema uongo. Wale waliozaliwa mara ya pili wako salama kama vile Mungu alivyo mwaminifu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page