Si Ya Kufurahisha vya Kutosha
- Dalvin Mwamakula
- Sep 2
- 1 min read

“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wezi huvunja na kuiba, bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji na kuiba. (Mathayo 6:19-20)
Ujumbe unaopaswa kupaziwa sauti kutoka kwenye nyumba za fedha za juu ni huu: Mwanadamu wa kidunia, hujatosheka kabisa na raha!
Acha kuridhika na mavuno kidogo ya 2% ya raha ambayo huliwa na nondo za mfumuko wa bei na kutu ya kifo. Wekeza katika dhamana za mbinguni zilizo na thamani kubwa, mavuno ya juu, na bima ya kimungu.
Kujitolea maisha kwa starehe za kimwili, usalama, na msisimko ni kama kutupa pesa kwenye shimo la panya.
Lakini kuwekeza maisha katika kazi ya upendo huzaa faida ya furaha isiyo na kifani na isiyo na mwisho:
“Uzeni mali zenu mkawape maskini. [Na hivyo ] jipatieni mifuko isiyochakaa, pamoja na hazina isiyoisha mbinguni” (Luka 12:33).
Ujumbe huu ni habari njema sana: Njooni kwa Kristo, ambaye mbele yake mna utimilifu wa furaha na raha milele. Jiunge nasi katika kazi ya Furaha ya Kikristo. Kwa maana Bwana amesema: Ni heri kupenda kuliko kuishi maisha ya anasa! Ubarikiwe zaidi sasa, na hata milele.




Comments