top of page

Simba na Mwanakondoo

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

“Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa. Hatagombana wala kupaza sauti, wala hakuna atakayesikia sauti yake katika njiani; Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, hadi atakapoleta haki ishinde. Katika jina lake Mataifa wataweka tumaini lao.” (Mathayo 12:18–21, akinukuu Isaya 42)


Nafsi ya Baba inafurahia kwa shangwe juu ya unyenyekevu na huruma ya Mwana wake kama mtumishi.

 

Mwanzi unapopinda na kukaribia kukatika, Mtumishi huyo ataushikilia wima mpaka upone. Wakati utambi unawaka kwa shida na hauna joto tena, Mtumishi hatauzima, bali ataufunika kwa mkono wake na kupuliza kwa upole hadi uwake tena.

 

Hivyo Baba analia, “Tazama, Mtumishi wangu ambaye nafsi yangu imependezwa naye!” Thamani na uzuri wa Mwana haukuja tu kutoka kwa ukuu wake, wala kutoka kwa upole wake tu, lakini kutoka kwa jinsi haya mawili yanavyo changanyika kwa uwiano kamili.

 

Malaika anapopaza sauti katika Ufunuo 5:2, “Ni nani astahiliye kuivunja hiyo mihuri na kukifungua kitabu?” jibu linarudi, “Usilie!; tazama, Simba wa kabila ya Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja mihuri yake saba” (Ufunuo 5:5).

 

Mungu anapenda nguvu za Simba wa Yuda. Hii ndiyo sababu anastahili machoni pa Mungu kufungua maandiko ya historia na kufunua siku za mwisho.

 

Lakini picha haijakamilika. Je, huyu Simba alishinda kwa namna ani? Mstari unaofuata unaeleza kuonekana kwake: “Na katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne na kati ya wale wazee nilimwona Mwana-Kondoo amesimama kana kwamba amechinjwa” (Ufunuo 5:6). Yesu anastahili furaha ya Baba si tu kama Simba wa Yuda, bali pia kama Mwana-Kondoo aliyechinjwa.

 

Huu ndio utukufu wa kipekee wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili - mchanganyiko wa kushangaza wa ukuu na unyenyekevu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page