top of page

Sisi Tunasubiri, Yeye Anatenda

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 30
  • 2 min read
ree

Tangu nyakati za zamani hakuna mtu aliyesikia, hakuna sikio lililotambua, hakuna jicho ambalo lililomwona Mungu mwingine ila wewe, anayetenda mambo kwa ajili ya wale mwangojeao. (Isaya 64:4)


Hakuna mambo mengi yaliyonifurahisha zaidi kuliko ukweli kwamba Mungu anapenda kuonyesha uungu wake kwa kunifanyia kazi, na kwamba kazi yake kwangu daima ni kabla na chini, na katika kazi yoyote ninayofanya kwa ajili yake.

 

Mwanzoni inaweza kuonekana kama tunajivuna, na kumdharau Mungu, kusema kwamba anafanya kazi kwa ajili yetu. Lakini hiyo ni kwa sababu tu ya dhana kwamba mimi ni mwajiri na Mungu anahitaji kazi. Hiyo sio maana wakati Biblia inazungumza juu ya kazi ya Mungu kwa ajili yetu. Hilo halipo kabisa akilini mwa Isaya anaposema, Mungu “hufanya kazi kwa ajili ya wale wanaomngoja” (Isaya 64:4).

 

Maana sahihi ya kusema Mungu ananifanyia kazi ni kwamba nimefilisika na ninahitaji dhamana. Mimi ni dhaifu na ninahitaji mtu mwenye nguvu. Niko hatarini na ninahitaji mlinzi. Mimi ni mjinga na ninahitaji mtu mwenye busara. Nimepotea na ninahitaji Mwokozi.

 

Mungu anapenda kuonyesha uungu wake kwa kunifanyia kazi, na kazi yake kwangu daima ni kabla, na chini, ndani, na katika  kazi yoyote ninayofanya kwa ajili yake.

Mungu ananifanyia kazi maana yake siwezi kufanya kazi hiyo. Nahitaji msaada kabisa.

 

Na hii inamtukuza Mungu sio mimi. Mtoaji anapata utukufu. Mwenye Nguvu anapata sifa.

 

Sikiliza jinsi Biblia inavyosema kuhusu Mungu kufanya kazi kwa ajili yako, na uwe huru kutokana na mzigo wa kubeba mzigo wako mwenyewe. Mwache afanye kazi hiyo.

 

  1. "Hakuna jicho lililomwona Mungu ila wewe, ambaye hufanya kazi kwa wale wanaomngoja" (Isaya 64: 4).


  2. Mungu "hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa kuwa yeye mwenyewe huwapa watu wote uzima na pumzi na kila kitu" (Matendo 17:25).


  3. “Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Marko 10:45).


  4. Kwa kuwa macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili kuwa tegemeza wale ambao mioyo yao ni  mikamilifu mbele zake.” (2 Mambo ya Nyakati 16:9)


  5. “Kama ningekuwa na njaa, nisingekuambia. . . . Uniite siku ya taabu; nitakuokoa, nawe utani-tukuza” (Zaburi 50:12,15).


  6. “Mpaka uzee wako . . . Nitakubeba. Mimi nimefanya, nami nitashikilia; nitabeba na kuokoa” (Isaya 46:4).


  7. “Nilifanya kazi kuliko wengine wote, ingawa si mimi, bali ni neema ya Mungu iliyo pamoja nami” (1 Wakorintho 15:10).


  8. “BWANA asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure” (Zaburi 127:1).


  9. “Yeyote anayetumikia, [na atumike] kwa nguvu anazo jaliwa na Mungu, ili Mungu atukuzwe katika kila jambo” (1 Petro 4:11).


  10. “Utimizeni wokovu wenu wenyewe . . . kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kufanya kazi pia” (Wafilipi 2:12–13).


  11. “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, lakini Mungu ndiye aliye kuza” (1 Wakorintho 3:6).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page