top of page

Tatizo la Kweli na Wasiwasi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 11
  • 1 min read
ree

Lakini ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yanaishi na kesho hutupwa motoni, je, hatawavika ninyi zaidi, enyi wa imani haba? (Mathayo 6:30)


Yesu anasema kwamba mzizi wa wasiwasi ni imani isiyotosheleza - "imani ndogo" - katika neema ya Baba yetu ya wakati ujao. 


Mwitikio mmoja kwa hili unaweza kuwa: “Hizi sio habari njema! Kwa kweli, inavunja moyo sana kujua kwamba kile nilichofikiri ni pambano tu na tabia ya wasiwasi ni pambano la kina zaidi la kujua kama ninamtumaini Mungu.”


Jibu langu kwa kukatishwa tamaa huku ni kukubaliana, lakini tena kutokubaliana. 


Tuseme ulikuwa unaumwa tumboni na umekuwa ukihangaika na dawa na vyakula vya kila aina, bila mafanikio. Na kisha tuseme kwamba daktari wako atakuambia, baada ya ziara ya kawaida, kwamba una saratani katika utumbo wako mdogo. Je, hiyo ingekuwa habari njema? Unasema, hapana! Na ninakubali.


Lakini wacha niulize swali kwa njia nyingine: Je, unafurahi kwamba daktari aligundua saratani hiyo ingali inatibika, na kwamba kwa hakika inaweza kutibiwa kwa mafanikio makubwa? Unasema, ndiyo, nimefurahi sana kwamba daktari amegunduwa tatizo halisi. Tena nakubali. 


Kwa hivyo, habari kwamba una saratani sio habari njema. Lakini, kwa maana nyingine, ni habari njema, kwa sababu kujua ni tatizo gani hasa ni jambo jema, hasa wakati tatizo lako linaweza kutibiwa kwa mafanikio.

Habari ya kuwa na saratani sio njema, lakini ni bora kujua tatizo halisi, hasa ikiwa linaweza kutibiwa kwa mafanikio.

Hivyo ndivyo inavyokuwa kujifunza kwamba tatizo halisi nyuma ya wasiwasi ni “imani ndogo” (kama Yesu anavyosema) katika ahadi za neema ya Mungu ya wakati ujao. Naye anaweza kufanya kazi kwa njia za ajabu za uponyaji tunapopaza sauti, “Naamini; nisaidie kutokuamini kwangu!” (Marko 9:24).



 
 
 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page