top of page

Tumaini Kuu la Kimishonari

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Oct 15
  • 2 min read
ree

Hata tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, [Mungu] alitufanya hai pamoja na Kristo — kwa neema mmeokolewa. (Waefeso 2:5)

 

Tumaini kuu la kimishonari ni kwamba wakati injili inapo hubiriwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe hufanya kile ambacho mwanadamu hawezi kufanya: anaunda imani inayookoa. Mwito wa Mungu hufanya kile ambacho mwito wa mwanadamu hauwezi. Unafufua wafu. Unatengeneza maisha ya kiroho. Ni kama wito wa Yesu kwa Lazaro kaburini, “Toka nje!” Na yule aliyekufa alitii na kutoka nje. Wito uliunda utii kwa kuunda maisha (Yohana 11:43). Hivyo ndivyo mtu yeyote anaokolewa.

 

Tunaweza kumwamsha mtu kutoka usingizini kwa sauti yetu, lakini sauti ya Mungu inaweza kuumba vitu ambavyo havipo (Warumi 4:17). Mwito wa Mungu hauzuiliki kwa maana unaweza kushinda upinzani wote. Ni yenye ufanisi usioweza kushindwa kulingana na kusudi la Mungu — kiasi kwamba Paulo anaweza kusema, “Wale aliowaita [Mungu] aliwahesabia haki pia” (Warumi 8:30), ingawa tunahesabiwa haki kwa imani yetu pekee.

 

Kwa maneno mengine, mwito wa Mungu ni wenye ufanisi kiasi kwamba huumba imani ambayo mtu huhesabiwa haki kupitia kwayo. Wote walioitwa wanahesabiwa haki kulingana na Warumi 8:30. Lakini hakuna anayehesabiwa haki bila imani (Warumi 5:1). Kwahiyo, mwito wa Mungu hauwezi kushindwa katika lengo lake liliyokusudiwa. Inaleta nguvu katika imani inayohesabia haki.

 

Hiki ndicho ambacho mwanadamu hawezi kufanya. Haiwezekani. Ni Mungu pekee anayeweza kuondoa moyo wa jiwe (Ezekieli 36:26). Ni Mungu pekee anayeweza kuwavuta watu kwa Mwana (Yohana 6:44, 65). Ni Mungu pekee anayeweza kufungua moyo uliokufa kiroho ili usikilize injili (Matendo 16:14). Ni Mchungaji Mwema pekee anayewajua kondoo wake, na huwaita kwa majina yao kwa nguvu ya kuvutia kiasi kwamba wote humfuata — na hawapotei kamwe (Yohana 10:3–4, 14). 

 

Neema kuu ya Mungu, inayofanya yasiyowezekana kwa wanadamu, kupitia injili ya Yesu Kristo, ndiyo tumaini kuu la kimishonari.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page