top of page

Tumaini kwa Wenye Dhambi WakuU Zaidi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 2
  • 1 min read
ree

“Nitamfadhili yeye nitakayemfadhili, nami nitamrehemu nitakayemrehemu.” (Kutoka 33:19)


Musa alihitaji tumaini kwamba Mungu kweli angeweza kuwa na huruma kwa watu wenye shingo ngumu ambao walikuwa wamefanya ibada ya sanamu na kumdharau Mungu aliyewatoa Misri. Ili kumpa Musa tumaini na ujasiri aliouhitaji, Mungu alisema, "Nitamrehemu yule nitakayemrehemu."


Kwa maneno mengine, “Chaguzi zangu hazitegemei kiwango cha uovu au wema ndani ya mwanadamu bali tu juu ya hiari yangu kuu. Kwa hiyo hakuna awezaye kusema kwamba yeye ni mwovu sana asiweze kuonyeshwa neema.” Hiyo inaweza kumaanisha Mungu hayuko huru, na uchaguzi hauna masharti.


Fundisho la uchaguzi usio na masharti ni fundisho kuu la tumaini kwa wadhambi wakubwa zaidi.


Ina maana kwamba inapokuja suala la kuwa mtarajiwa wa neema, historia yako haina uhusiano wowote na chaguo la Mungu. Hiyo ni habari njema.

Ikiwa hujazaliwa mara ya pili na kuletwa kwenye imani iokoayo katika Yesu Kristo, usizame katika kukata tamaa ukifikiri kwamba uozo au ugumu wa maisha yako ya zamani ni kizuizi kisichoweza kushindwa kwa kazi ya neema ya Mungu katika maisha yako. Mungu anapenda kukuza uhuru wa neema yake kwa kuwaokoa wale wanaonekana ndio wadhambi wakubwa zaidi.


Geuka kutoka katika dhambi yako; mwite Bwana. Hata katika ibada hii ya kila siku, ambayo unasoma au kusikia, yeye anakuwa na neema kwako, na anakupa moyo mkubwa wa kuja kwake kwa ajili ya rehema. 


“Njooni, tusemezane, asema Bwana; dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu” (Isaya 1:18).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page