Tumehesabiwa Haki Kikamilifu
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 2 min read

Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye anayehesabia haki. (Warumi 8:33)
Paulo angeweza kusema hapa, “Ni nani atakayeleta mashtaka dhidi ya wateule wa Mungu?” kisha akajibu, “Hakuna mtu! Tumehesabiwa haki.” Hiyo ni kweli. Lakini sivyo alivyosema. Jibu lake badala yake ni, “Mungu ndiye mwenye kuhesabia haki.”
Msisitizo hauko kwenye kitendo bali kwa Anayetenda.
Kwanini? Kwasababu katika ulimwengu wa mahakama na sheria ambapo lugha hii inatoka, kuachiliwa kwa hakimu kunaweza kubatilishwa na aliye juu zaidi.
Kwa hivyo, itakuaje ikiwa hakimu wa eneo hilo atakuachilia, wakati una hatia, ikiwa gavana ana haki ya kuleta mashtaka dhidi yako? Basi itakuwaje, ikiwa gavana atawaweka huru, mkiwa na hatia, ikiwa mfalme anaweza kuleta mashtaka dhidi yenu?
Hakuna mahakama juu ya Mungu. Mungu akikusamehe na kukutangaza mwadilifu, hakuna rufaa au makosa yanayoweza kutafutwa dhidi yako. Hukumu ya Mungu ni ya mwisho.
Jambo kuu hapa ni: Juu ya Mungu, hakuna mahakama za juu zaidi. Ikiwa Mungu ndiye anayekusamehe — anakutangaza kuwa mwadilifu machoni pake — hakuna awezaye kukata rufaa; hakuna mtu awezaye kuitisha hukumu; hakuna anayeweza kutafuta makosa mengine dhidi yako. Hukumu ya Mungu ni ya mwisho na ya jumla.
Sikieni haya, ninyi nyote mnaomwamini Yesu, na kuunganishwa na Kristo, na kujionyesha wenyewe kati ya wateule: Mungu ndiye anayewahesabia haki. Sio mwamuzi wa kibinadamu. Si nabii mkuu. Sio malaika mkuu kutoka mbinguni. Lakini Mungu, Muumba wa ulimwengu na Mmiliki wa vitu vyote na Mtawala wa ulimwengu na kila molekuli na mtu ndani yake, Mungu ndiye anayekuhesabia haki.
Hoja: usalama usiotikisika katika uso wa mateso makubwa. Ikiwa Mungu yuko upande wetu, hakuna anayeweza kufanikiwa kuwa dhidi yetu. Ikiwa Mungu alimtoa Mwana wake kwa ajili yetu, atatupatia kila kitu ambacho ni kizuri kwa ajili yetu. Ikiwa Mungu ndiye anayetuhesabia haki, hakuna mashtaka dhidi yetu yanayoweza kusimama.




Comments