Tunafanya kazi kwa Neema
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 2 min read

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. (1 Wakorintho 15:10)
Paulo alitambua kwamba sehemu ya kwanza ya mstari huu inaweza isieleweke: “Nilifanya kazi kwa bidii kuliko yeyote kati yao.” Kisha anaendelea kusema, “Ingawa sio mimi, bali ni neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.”
Paulo haunganishi utii wake na shukrani kwa neema ya zamani. Badala yake, anauelekeza kwa neema inayokuja kila wakati—neema ya kila muda, isiyokoma kufika. Anategemea ahadi ya neema ya baadaye ya Mungu kufika kila mara anapohitaji msaada. Katika kila sekunde ya nia na jitihada za Paulo kumtii Kristo, neema ilikuwa ikifanya kazi ili kuleta nia hiyo na jitihada hizo. Paulo hakufanya kazi yake kwa msingi wa shukrani tu kwa neema iliyopita, bali kwa kutegemea kila wakati kuwasili kwa neema aliyoahidiwa. Paulo anataka kusisitiza kwamba neema ya Mungu inayowasili kila mara ndiyo sababu kuu ya kazi yake.
Je, inasema hivyo kweli? Je, haisemi tu kwamba neema ya Mungu ilifanya kazi pamoja na Paulo? Hapana, inasema zaidi. Inatubidi tukubaliane na maneno, “Ingawa sio mimi.” Paulo anataka kuinua neema ya Mungu ya muda baada ya muda kwa namna ambayo ni wazi kwamba yeye mwenyewe sio mwamuzi na mtendaji mkuu wa kazi hii.
Hata hivyo, yeye ni mtendaji wa kazi hii: “Nilifanya kazi kwa bidii kuliko yeyote kati yao.” Alifanya kazi. Lakini alisema ilikuwa ni neema ya Mungu “juu yangu.”
Neema ndiye mwamuzi mkuu katika huduma ya Paulo, ikimpa nguvu ya kutekeleza kazi yake.
Tukiacha sehemu zote za mstari huu zisimame, matokeo ya mwisho ni haya: neema ndio mwamuzi atendaye katika kazi ya Paulo. Kwa kuwa Paulo pia ni mtendaji wa kazi yake, jinsi neema inavyokuwa mtendaji mkuu ni kwa kuwa nguvu wezeshi ya kazi ya Paulo.
Nachukua hili kumaanisha kwamba, Paulo alipokabiliana na mzigo wa huduma ya kila siku, aliinamisha kichwa chake na kukiri kwamba, isipokuwa neema ya wakati ujao ingetolewa kwa kazi ya siku hiyo, hangeliweza kuifanya.
Labda alikumbuka maneno ya Yesu, “Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yohana 15:5). Kwa hiyo aliomba kwa ajili ya neema ya wakati ujao kwa ajili ya siku hiyo, na aliamini katika ahadi kwamba ingekuja kwa nguvu. “Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu” (Wafilipi 4:19).
Kisha akatenda kwa nguvu zake zote.




Comments