Udhaifu Wetu Unadhihirisha Ustahili Wake
- Dalvin Mwamakula
- Jul 31
- 1 min read

"Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu." (2 Wakorintho 12:9)
Mpango wa Mungu kwa ajili ya mateso ni kwamba yanapaswa kukuza thamani na nguvu za Kristo. Hii ni neema, kwa sababu furaha kuu ya Wakristo ni kumwona Kristo akitukuzwa katika maisha yetu.
Wakati Paulo alipoambiwa na Bwana Yesu kwamba “mwiba katika mwili” wake hautaondolewa, alimsaidia Paulo kuimarisha imani yake kwa kueleza sababu. Bwana alisema, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hukamilishwa katika udhaifu” (2 Wakorintho 12:9). Mungu amepanga kwamba Paulo awe dhaifu ili Kristo aonekane kuwa mwenye nguvu kwa niaba ya Paulo.
Ikiwa tunajisikia na kuonekana kujitosheleza, sisi tutapata utukufu, si Kristo. Kwa hivyo, Kristo huchagua vitu dhaifu vya ulimwengu "ili mwanadamu yeyote asijisifu mbele za Mungu" (1 Wakorintho 1:29). Na wakati mwingine huwafanya watu wanaoonekana kuwa na nguvu kuwa dhaifu ili nguvu ya kimungu idhihirike zaidi.
Tunajua kwamba Paulo aliiona hii kama neema kwa sababu aliifurahia: “Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Hii ndiyo sababu, kwa ajili ya Kristo, nafurahia udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso na katika shida, kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu.” (2 Wakorintho 12:9–10).
Kuishi kwa imani katika neema ya Mungu kunamaanisha kuridhika na yote ambayo Mungu ni kwa ajili yetu ndani Yesu Kristo.
Kwa hiyo, imani haitarudi nyuma kutoka kwa kile kinachofunua na kukuza yote ambayo Mungu ni kwa ajili yetu ndani ya Yesu Kristo. Hivyo ndivyo udhaifu wetu wenyewe na mateso yetu yanakusudiwa kufanya kazi.




Comments