UHAKIKA wa Maombi
- Dalvin Mwamakula
- Feb 26
- 2 min read

Ahadi zote za Mungu zinapata Ndiyo yao ndani yake. Ndiyo maana ni kupitia kwake tunasema Amina yetu kwa Mungu kwa utukufu wake. (2 Wakorintho 1:20)
Maombi ni jibu au mwitikio kwa ajili ya ahadi, yaani, uhakikisho wa neema ya Mungu ya baadaye.
Maombi ni kuchukua kutoka kwenye akaunti ambayo Mungu ameweka hazina zake zote za neema ya baadaye.
Maombi si kutumaini bila sababu kwamba kunaweza kuwa na Mungu mwenye nia njema huko nje. Maombi yanategemea ahadi ya Mungu, na kila siku yanaenda benki na kuchukua hazina za neema ya baadaye zinazohitajika kwa ajili ya siku hiyo.
Usikose uhusiano kati ya nusu mbili za mstari huu mzuri. Angalia “ndiyo maana”: “Ahadi zote za Mungu ni Ndiyo katika Kristo. Ndiyo maana tunasema Amina kupitia kwake, kwa utukufu wa Mungu.”
“Amina” inamaanisha, “Ndiyo, Mungu ametoa ahadi hizi zote.” Inathibitisha uwezo, hekima, huruma, na neema ya Mungu, na ni ishara ya matumaini na ujasiri baada ya sala.
Ili kuhakikisha tunaona, hebu tugeuze hizi nusu mbili: Tunapoomba, tunasema Amina kwa Mungu kupitia Kristo, kwasababu Mungu amesema Amina ya uamuzi kwa ahadi zake zote katika Kristo. Maombi ni ombi la kujiamini kwa Mungu kutimiza ahadi zake za neema ya baadaye — kwa ajili ya Kristo. Maombi yanaunganisha imani yetu katika neema ya baadaye na msingi wa yote, Yesu Kristo.
Hii inatupeleka kwenye hoja ya mwisho: “Amina” ni neno kamili na lenye thamani wakati wa maombi. Haimaanishi hasa, “Ndio, sasa nimesema ombi hili.” Inamaanisha kimsingi, “Ndiyo, Mungu ametoa ahadi hizi zote.”
Amina inamaanisha, “Ndiyo, Bwana, unaweza kufanya hivyo.” Inamaanisha, “Ndiyo, Bwana, wewe ni mwenye nguvu. Ndiyo, Bwana, wewe ni mwenye hekima. Ndiyo, Bwana, wewe ni mwenye huruma. Ndiyo, Bwana, neema yote ya baadaye inatoka kwako na imethibitishwa katika Kristo."
"Amina" ni alama ya matumaini na ujasiri wa haki baada ya sala ya msaada.




Comments