top of page

Ujuzi wa Kweli Huleta Furaha Kubwa Zaidi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 1 min read

Updated: May 1

ree

Na watu wote wakaenda zao. . . kufanya furaha kubwa, kwa sababu walikuwa wameelewa maneno ambayo walikuwa wameambiwa. (Nehemia 8:12)


Furaha pekee inayoakisi thamani ya Mungu na kufurika katika upendo wa kumtukuza Mungu imejikita katika marifa ya kweli kuhusu Mungu. Na kwa kadri marifa yetu yalivyo madogo au yenye dosari, furaha yetu itakuwa mwangwi mbaya wa ubora wa ukweli wa Mungu.

 

Uzoefu wa Israeli katika Nehemia 8:12 ni kielelezo cha jinsi furaha ya kumtukuza Mungu hutokea moyoni. Ezra alikuwa amewasomea neno la Mungu na Walawi walikuwa wamewaelezea. Na kisha watu wakaenda zao “ili kushangilia sana.”

 

Furaha yetu lazima itokane na maarifa ya kweli ya utukufu wa Mungu ili kuakisi utukufu wake. Ili kumfurahia Mungu ipasavyo, ni lazima tumjue kweli.

Furaha yao kuu ilikuwa kwa sababu walikuwa wameelewa maneno - maneno ya kweli ya Mungu. Wengi wetu tumeonja uzoefu huu wa moyo kuwaka kwa furaha wakati neno la Mungu lilipofunguliwa kwetu (Luka 24:32). Mara mbili Yesu alisema kwamba aliwafundisha wanafunzi wake kwa ajili ya furaha yao.

 

  • Yohana 15:11 "Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu iwe kamili."

  • Yohana 17:13 , “Haya nayanena ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu ikamilike ndani yao.”

 

Na kile tunachokiona hasa katika neno hili ni Bwana mwenyewe - Mungu mwenyewe - akijitoa mwenyewe kujulikana na kufurahiwa. "Bwana alijifunua kwa Samweli huko Shilo kwa Neno la Bwana" (1 Samweli 3:21).

 

Jambo kuu ni kwamba ikiwa furaha yetu itaakisi utukufu wa Mungu, basi lazima itiririke kutokana na maarifa ya kweli ya jinsi gani Mungu alivyo mtukufu. Ikiwa tutamfurahia Mungu ipasavyo, ni lazima tumjue kweli ikweli.


 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page