top of page

Ukuaji wa Kanisa Kwa Njia ya Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Ibrahimu. (Warumi 9:8)


Mfikirie Ibrahimu wa Agano la Kale kama mchungaji. Bwana anasema, “Nitakubariki na kufanikisha huduma yako.” Lakini kanisa ni tasa na halizai watoto.

 

Ibrahimu anafanya nini? Anaanza kukata tamaa juu ya nguvu ya kiungu kuweza kuingilia kati. Anazeeka. Mkewe anabaki tasa. Kwa hiyo anaamua kumleta mwana aliyehaidiwa na Mungu bila nguvu za kiungu. Anafanya ngono na Hagari kijakazi wa mkewe (Mwanzo 16:4). Hata hivyo, matokeo si “mtoto wa ahadi,” bali “mtoto wa mwili,” Ishmaeli.

 

Mungu anamshangaza Ibrahimu kwa kusema, “Nitakupa mwana kwa yeye [mke wako Sara]” (Mwanzo 17:16). Kwa hiyo Ibrahimu akamlilia Mungu, “Laiti Ishmaeli angeishi mbele yako!” (Mwanzo 17:18). Anataka kazi ya bidii yake ya asili, ya kibinadamu iwe utimizo wa ahadi ya Mungu. Lakini Mungu anasema, “La, hapana! lakini Sara mkeo atakuzalia mwana” (Mwanzo 17:19). 

 

Lakini Sarah ana umri wa miaka 90. Amekuwa tasa maisha yake yote, na tayari amepitia katika kukoma hedhi (Mwanzo 18:11). Ibrahimu ana miaka 100. Tumaini pekee kwa mtoto wa ahadi ni muujiza wa kushangaza wa kiungu. 

 

Hiyo ndiyo maana ya kuwa "mtoto wa ahadi" - kuzaliwa "si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu" (Yohana 1:13). Watoto pekee wanaohesabiwa kuwa watoto wa Mungu katika ulimwengu huu ni watoto waliozaliwa kwa njia nguvu ya kiungu  ya ahadi. Katika Wagalatia 4:28 Paulo anasema, “Ninyi [Wakristo], kama Isaka, mmekuwa wana wa ahadi.” "Umezaliwa kwa Roho," si kwa jinsi ya mwili (Wagalatia 4:29). 

 

Mfikirie Ibrahimu kama mchungaji tena. Kanisa lake halikui katika namna anavyoamini Mungu ameahidi. Amechoka kusubiri muujiza wa kiungu. Anamgeukia “Hagari” kwa mbinu za kibinadamu tu, na anaamua kuwa anaweza “kuvutia watu” bila kazi ya nguvu ya kiungu ya Roho Mtakatifu. 

 

Hata hivyo, haitakuwa kanisa la Isaka, lakini Waishmaeli - watoto wa mwili, sio watoto wa Mungu. Mungu atuepushe na aina hii ya mafanikio mabaya.

Kwa vyovyote vile, fanya kazi. Lakini daima mtazame Bwana kwa ajili ya kazi ya kimiujiza yenye maamuzi kamili.

“Farasi huandaliwa kwa siku ya vita, bali ushindi ni wa Bwana.” (Mithali 21:31).

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page