Unakubali Kushindwa na Dhambi ya Zinaa, Kwasababu...
- Dalvin Mwamakula
- Jul 31
- 1 min read

Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.
. . . . Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze. (Zaburi 51:8,12)
Kwa nini Daudi halalamiki juu ya kujizuia kingono? Kwa nini haombi watu wamshike katika uwajibikaji? Kwa nini haombi macho yaliyohifadhiwa na mawazo yasiyojaa ngono? Katika zaburi hii ya ungamo na toba baada ya kimsingi kumbaka Bathsheba, mtu angeweza kutarajia Daudi aombe mambo kama hayo.
Sababu ni kwamba anajua kwamba dhambi ya zinaa ni dalili, si ugonjwa wenyewe.
Watu wanakubali kushindwa na dhambi za kingono kwa sababu hawana utimilifu wa furaha na shangwe katika Kristo.
Roho zao hazijasimama imara na thabiti na hazijaimarishwa. Wanatetereka. Wanarubuniwa, na wanakubali kwa sababu Mungu hana nafasi ya juu katika hisia na mawazo yao kama anavyopaswa kuwa.
Daudi alijua hili kujihusu mwenyewe. Ni kweli kuhusu sisi pia. Daudi anatufundisha, kwa jinsi anavyoomba, hitaji la kweli kwa wale wanaotenda dhambi ya zinaa: Mungu! Furaha katika Mungu.
Hii ni hekima ya kina kwetu.




Comments