top of page

Upendo wa Bure

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

ree

“Tazama, mbingu na mbingu za mbingu ni za Bwana, Mungu wako, na dunia pamoja na vyote vilivyomo. Lakini Bwana aliuelekeza moyo wake kwa baba zenu na kuwachagua wazao wao baada yao, ninyi zaidi ya mataifa yote kama mlivyo hivi leo.” (Kumbukumbu la Torati 10:14–15)


Upendo wa Mungu unaochagua—upendo ambao kwao huchagua watu kwa ajili yake mwenyewe—ni bure kabisa. Ni kufurika kwa neema ya furaha yake isiyo na mipaka inayoongozwa na hekima yake isiyo na mwisho.


Kumbukumbu la Torati 10:14–15 inaelezea furaha ambayo Mungu alikuwa nayo katika kuchagua Israeli kutoka kwa watu wote wa dunia. Tambua vitu viwili.


Kwanza, ona tofauti kati ya aya ya 14 na 15. Kwa nini Musa anaelezea kuchaguliwa kwa Israeli dhidi ya hali ya nyuma ya umiliki wa Mungu wa ulimwengu mzima? Kwa nini anasema katika mstari wa 14, “Kila kitu mbinguni na duniani ni cha Mungu” na kisha kusema katika mstari wa 15, “Hata hivyo aliwachagua ninyi kuwa watu wake”?


Sababu inaonekana kuwa ni kuondoa dhana yoyote kwamba Mungu kwa namna fulani aliwekwa katika kuchagua watu hawa - kwamba kulikuwa na mipaka kwa uchaguzi wake na kwa namna fulani alilazimishwa kuwachagua. Hoja ni kulipuwa wazo la kipagani kwamba mungu anaweza kuwa na haki na mamlaka ya kuwa na watu wake lakini sio hivyo tena.


Ukweli ni kwamba Yehova ndiye Mungu wa pekee wa kweli. Anamiliki kila kitu katika ulimwengu na ana haki na mamlaka ya kuchukua watu wowote anaowataka kwa milki yake maalum.


Hivyo ukweli wa ajabu usioelezeka kwa Israeli ni kwamba aliwachagua wao. Hakulazimika kufanya hivyo. Alikuwa na haki na mapendeleo ya kuchagua kabisa watu wowote juu ya uso wa dunia kwa makusudi yake ya ukombozi. Au wao wote. Au hakuna hata mmoja wao.


Kwa hiyo, anapojiita “Mungu wao” haimaanishi kwamba yuko sawa na miungu ya Misri au miungu ya Kanaani. Anamiliki miungu hiyo na watu wao. Ikiwa ingempendeza, angaliweza kuchagua watu tofauti kabisa ili kutimiza makusudi yake.


Jambo la kuunganisha mistari ya 14 na 15 kwa njia hii ni kusisitiza uhuru na haki na mamlaka ya Mungu ya ulimwengu mzima.


Jambo la pili la kuona (katika mstari wa 15) ni jinsi Mungu anavyotumia uhuru wake wa enzi kuu “kuweka moyo wake katika upendo kwa baba zako.” "Alipendezwa na baba zako kuwapenda." Alichagua kwa hiari kufurahia kuwapenda mababa.


Upendo wa Mungu kwa wababa wa Israeli ulikuwa huru na wa rehema na haukulazimshwa na chochote ambacho mababa walikuwa katika uyahudi wao au katika wema wao.


Hili ni somo kwetu. Kwa sisi ambao ni waamini katika Kristo:


Mungu ametuchagua sisi bure. Si kwa sababu ya kitu chochote ndani yetu, lakini kwa sababu Mungu alifurahia tu kufanya hivyo.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page