top of page

Usimtumikie Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 28
  • 2 min read

Updated: May 1

ree

“Kwa kuwa macho ya BWANA hukimbiakimbia duniani kote, ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea yeye kwa ukamilifu.” (2 Mambo ya Nyakati 16:9)


Mungu anatafuta nini duniani? Wasaidizi? Hapana. Injili sio bango linalosema "msaada unahitajika". Wala mwito wa huduma ya Kikristo.


Mungu hatafuti watu wa kumfanyiaa kazi yake. Kwa kuwa macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili kujionyesha mwenye nguvu wale ambao mioyo yao ni  mikamilifu mbele zake.” (2 Mambo ya Nyakati 16:9) Yeye ndiye mfanyakazi mkuu. Yeye ndiye mwenye mabega mapana, yenye kubeba mizigo mizito. Yeye ndiye mwenye nguvu. Na anatafuta njia za kuionyesha. Hiki ndicho kinachomtofautisha Mungu na wale wanaoitwa miungu wa ulimwengu: anafanya kazi kwa ajili yetu. Isaya 64:4, “Tangu zamani hakuna aliyesikia wala kutambua kwa sikio, wala hakuna jicho lililomwona Mungu ila wewe [kwa maneno mengine huu ni upekee wake], ambaye hufanya kazi kwa ajili ya wale wanaomngoja.”


Mungu anataka nini kutoka kwetu? Si kile tunachoweza kutarajia. Anakemea Israeli kwa kumletea dhabihu nyingi sana: “Sitapokea fahali kutoka nyumbani mwako. . . . Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu. . . . 'Kama ningalikuwa na njaa, nisingekuambia, kwa maana ulimwengu na vyote viijazavyo ni wangu'” (Zaburi 50:9–10,12).


Lakini je, hakuna kitu tunachoweza kumpa Mungu ambacho hakitamshusha hadhi na kumfanya mfadhiliwa?
Kipo. Wasiwasi wetu. Mahitaji yetu. Vilio vyetu vya kuomba uwezo wa kufanya mapenzi yake.

Ni amri: “[Mtwikeni] yeye fadhaa zenu zote” (1 Petro 5:7). Mungu atapokea kwa furaha chochote kutoka kwetu ambacho kinaonyesha utegemezi wetu na utoshelevu wake wote.


Ukristo kimsingi ni kupona baada ya ugonjwa. Wagonjwa hawahudumii matabibu wao. Wanawaamini kwa ajili ya maagizo na tiba nzuri. Mahubiri ya Mlimani ni utaratibu wa matibabu wa Daktari wetu, sio maelezo ya kazi ya Mwajiri wetu.


Maisha yetu yanategemea sio kumfanyia Mungu kazi. “Kwa mtu anayefanya kazi, mshahara wake hauhesabiwi kuwa ni zawadi, bali ni haki yake. Na kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye huwahesabia haki waovu, imani yake imehesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:4-5).


Wafanyakazi hawapati zawadi. Wanapata haki yao. Mshahara wao. Kama tungekuwa na zawadi ya kuhesabiwa haki, hatuthubutu kuifanyia kazi. Mungu ndiye mtenda kazi katika jambo hili. Na anachopata ni utukufu wa kuwa mfadhili wa neema, sio mnufaika wa huduma.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page