top of page

Usiogope Kifo Tena

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read

ree

Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi, na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti. (Waebrania 2:14-15)


Kristo anatukomboaje kutoka kwenye hofu ya kifo na kutuweka huru kuishi kwa upendo wa kujitolea ambao unaweza “kuacha mali na ndugu, maisha haya ya kifo pia”?

 

Kwa kuwa watoto wana damu na nyama . . .

 

Neno “watoto” limechukuliwa kutoka katika mstari uliotangulia na inamaanisha uzao wa kiroho wa Kristo, Masihi. Hawa pia ni “watoto wa Mungu.” Kwa maneno mengine, katika kumtuma Kristo, Mungu anafikiria hasa wokovu wa "watoto" wake. “Kwa kuwa watoto wana damu na nyama . . . ”

 

yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao. . .

 

Mwana wa Mungu, ambaye alikuwepo kabla ya kufanyika mwili kama Neno la milele (Yohana 1:1), alivaa mwili na damu, na kuuvika uungu wake ubinadamu. Akawa mwanadamu kamili na kubaki kuwa Mungu kamili. 

 

ili kwa kifo chake. . .

 

Sababu ya Kristo kufanyika mwanadamu ilikuwa ni kufa. Kama Mungu kabla ya kuvaa mwili na damu, hangeweza kufa kwa ajili ya wenye dhambi. Lakini akiunganishwa na nyama na damu, angeliweza. Lengo lake lilikuwa kufa. Kwa hiyo, ilimbidi azaliwe mwanadamu, mwenye kufa. 

 

apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi. . .

 

Katika kufa, Kristo alimnyang’anya ibilisi nguvu. Kivipi? Kwa kufunika dhambi zetu zote (Waebrania 10:12). Hii ina maana kwamba Shetani hana sababu halali ya kutushtaki mbele za Mungu. “Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye ahesabiaye haki” (Warumi 8:33). Je, anatuhesabia haki kwa misingi gani? Kupitia damu ya Yesu (Waebrania 9:14; Warumi 5:9).

 

Silaha kuu ya Shetani dhidi yetu ni dhambi zetu wenyewe. Ikiwa kifo cha Yesu huiondoa, silaha kuu aliyo nayo shetani itatolewa mkononi mwake. Kwa maana hiyo, anakuwa hana uwezo. 

 

na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti

 

Kwa hiyo, tuko huru kutokana na hofu ya kifo. Mungu ametuhesabia haki. Kuna neema ya baadaye tu mbele yetu. Shetani hawezi kupindua shauri hilo. Na Mungu anakusudia usalama wetu wa mwisho kuwa na matokeo ya haraka kwenye maisha yetu. Anamaanisha mwisho mwema kuondoa utumwa na woga wa sasa.


Kwa hiyo, tuko huru kutokana na hofu ya kifo. Mungu ametuhesabia haki. Kuna neema ya baadaye tu mbele yetu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page