top of page

Uzima na Kifo wakati wa Krismasi

  • Writer: Joshua Phabian
    Joshua Phabian
  • 4 days ago
  • 2 min read
ree

  

“Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu. mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele.” (Yohana 10:10)


Nilipokuwa karibu kuanza ibada hii, nilipokea taarifa kwamba Marion Newstrum alikuwa amekufa. Marion na mume wake Elmer walikuwa wamekuwa sehemu ya kanisa letu kwa muda mrefu zaidi kuliko wengi wa washirika wetu walivyokuwa hai wakati huo. Alikuwa na umri wa miaka 87. Walikuwa wameoana kwa miaka 64.


Nilipozungumza na Elmer na kumwambia nilitaka awe na nguvu katika Bwana na asikate tamaa maishani, alisema, “Amekuwa rafiki wa kweli.” Ninaomba kwamba Wakristo wote wataweza kusema mwishoni mwa maisha, “Kristo amekuwa rafiki wa kweli.” 


Ukiwa na uchungu huleta hadhari ya kujidhuru mwenyewe.

Kila Majilio ninaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mama yangu. Alikatishwa katika mwaka wake wa 56 katika ajali ya basi huko Israel. Ilikuwa Desemba 16, 1974. Matukio hayo ni halisi kwangu hata leo. Nikijiruhusu, naweza kutokwa na machozi kwa urahisi - kwa mfano, nikifikiria kwamba wanangu hawakumjua kamwe. Tulimzika siku iliyofuata Krismasi. Ilikuwa Krismasi yenye thamani kama nini!


Wengi wenu mtahisi upotevu wenu Krismasi hii kwa uwazi zaidi kuliko hapo awali. Usiizuie. Ruhusu zije. Zihisi. Upendo ni wa nini, ikiwa sio kuongeza mapenzi yetu - katika uzima na kifo? Lakini ah, usiwe na uchungu. Ukiwa na uchungu huleta hadhari ya kujidhuru mwenyewe.


Yesu alikuja wakati wa Krismasi ili tupate uzima wa milele. “Mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Elmer na Marion walikuwa wamejadili mahali wangemalizia miaka yao ya mwisho. Elmer alisema, “Mimi na Marion tulikubaliana kwamba nyumba yetu ya mwisho itakuwa na Bwana.”


Je, unahisi kukosa utulivu nyumbani? Nina familia inayokuja nyumbani kwajili likizo. Hujisikia vizuri. Nadhani sababu ya msingi kwa nini inapendeza ni kwamba mimi na wao tumekusudiwa katika kina cha uhai wetu kwa Kurudi Nyumbani kwa mwisho. Kurudi nyumbani kwa wengine wote ni mwonjo wa awali. Na mwonjo wa awali ni mzuri.


Isipokuwa wanakuwa mbadala. Lo, usiruhusu mambo yote matamu ya msimu huu yawe mbadala wa Utamu wa mwisho, mzuri na wa kuridhisha. Hebu kila ulichopoteza na kila furaha zipeleke mioyo yenu katika mbingu.


Krismasi. Ni nini isipokuwa hii: Mimi nalikuja ili wawe na uzima ? Marion Newstrum, Ruth Piper, na wewe na mimi - ili tuwe na Uzima, sasa na hata milele.


Ifanye Sasa yako kuwa tajiri zaidi na zaidi Krismasi hii kwa kunywa kwenye chemchemi ya Milele . Iko karibu sana.


Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page