Uzito wa Shukrani
- Dalvin Mwamakula
- Nov 14
- 1 min read

Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za taabu. Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kiburi, wenye majivuno, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani . . . (2 Timotheo 3:1-2)
Angalia jinsi kutokuwa na shukrani kunavyoambatana na kiburi, unyanyasaji, na kutotii.
Katika sehemu nyingine Paulo anasema, “Kusiwe na uchafu wala mazungumzo ya kipumbavu wala mzaha usiofaa . . . bali badala yake kuwe na shukrani” (Waefeso 5:4). Kwa hiyo, inaonekana kwamba shukrani, kushukuru, ni kinyume cha ubaya na vurugu.
Sababu ya hii ni kwamba hisia ya shukrani ni hisia ya unyenyekevu, sio ya kiburi. Ni kukweza wengine, sio kujikweza. Na ni furaha ya moyo, sio hasira au uchungu. Kushukuru kwa uchungu ni kupingana kwa maneno.
Ufunguo wa kufungua moyo wa shukrani na kushinda uchungu, ubaya, ukosefu wa heshima, na jeuri ni imani yenye nguvu katika Mungu, Muumba na Mlinzi na Mpaji na Mtoa Matumaini.
Ikiwa hatuamini kwamba tuna deni kubwa kwa Mungu kwa yote tuliyo nayo na tunayotumaini kuwa nayo, basi chemchemi ya shukrani imekauka.
Kwa hivyo, ninahitimisha kwamba kuongezeka kwa vurugu na kufuru na ubaya na ukaidi katika nyakati za mwisho ni suala linalomhusu Mungu. Suala la msingi ni kushindwa kuhisi shukrani katika viwango vya juu vya utegemezi wetu.
Wakati chemchemi ya juu ya shukrani kwa Mungu inapokauka kwenye kilele cha mlima, mda si mrefu vidimbwi vyote vya shukrani huanza kukauka chini ya mlima. Na shukrani inapokwisha, ukuu wa nafsi hukubali na kuidhinisha uharibifu zaidi na zaidi kwa ajili ya raha yake.
Omba kwa ajili ya mwamko mkuu wa shukrani ya unyenyekevu.




Comments