Vitambaa Vichafu Hakuna Tena
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 2 min read
Updated: May 1

Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu. (Isaya 64:6)
Ni kweli kwamba kushindwa kokote kuitii sheria ya Mungu kunakosea utakatifu wake mkamilifu na kunatufanya kustahili hukumu, kwa sababu Mungu hawezi kukubali dhambi yoyote. (Habakuki 1:13; Yakobo 2:10-11).
Lakini kilichomwangamiza mtu katika Agano la Kale (na hali ni vivyo hivyo kwetu leo) haikuwa kushindwa kuwa na haki ya ukamilifu usio na dhambi. Kilichowaletea maangamizi ni kutokumwamini Mungu na ahadi zake za rehema, hasa tumaini kwamba siku moja atamtoa Mkombozi ambaye atakuwa haki kamilifu kwa ajili ya watu wake (“BWANA ni haki yetu,” Yeremia 23:6 33:16).
Watakatifu wa Agano la Kale walijua kwamba hivi ndivyo walivyookolewa, na kwamba imani hii ilikuwa ufunguo wa utii, na kwamba utii huo ulikuwa ushahidi wa imani hii.
Inachanganya sana watu wanaposema kwamba haki pekee yenye thamani yoyote ni ile haki ya Kristo tuliyohesabiwa. Ni kweli kwamba kuhesabiwa haki kwetu hakutokani kamwe na haki yetu sisi wenyewe—hata kama ni haki ambayo Roho ameizalisha ndani yetu kwa imani—bali hutegemea tu haki ya Kristo tuliyohesabiwa. Lakini wakati mwingine watu hawajali na wanaidharau haki yoyote ya kibinadamu, kana kwamba hakuna kabisa haki inayozalishwa ndani yetu inayompendeza Mungu. Hii siyo sawa wala haisaidii.
Mara nyingi wao hutaja Isaya 64:6, inayosema uadilifu wetu ni kama tambaa chafu, au “vazi lililo najisi.”
Lakini katika muktadha, Isaya 64:6 haimaanishi kwamba haki yote inayotendwa na watu wa Mungu haikubaliki mbele za Mungu. Isaya hapa anazungumzia watu ambao haki yao kwa hakika ni ya kinafiki, na hivyo si haki tena. Lakini katika mstari mmoja tu kabla ya huu, Isaya anasema kwamba Mungu kwa ridhaa hukutana na “yeye atendaye haki kwa furaha.” (Isaya 64:5).
Ni kweli - ukweli wa utukufu - kwamba hakuna hata mmoja wa watu wa Mungu, kabla au baada ya msalaba, ambaye angekubaliwa na Mungu mtakatifu ikiwa haki kamilifu ya Kristo haingehesabiwa kwetu (Warumi 5:19 ; 1 Wakorintho 1:30; 2) Wakorintho 5:21). Hiyo ni kweli! Lakini hiyo haimaanishi kwamba Mungu hazalishi ndani ya watu hao "waliohesabiwa haki" haki ya uzoefu ambayo sio "vazi lililochafuliwa" - ingawa bado haijakamilishwa.
Kwa kweli, yeye huzalisha haki kama hiyo, na haki hii ni ya thamani kwa Mungu na, kwa kweli, inahitajika—sio kama msingi wa kuhesabiwa haki kwetu (ambayo ni haki ya Kristo pekee), bali kama uthibitisho wa kuwa watoto wa Mungu waliohesabiwa haki kweli. Hiki ndicho ambacho Paulo anaomba, nasi tunapaswa kukiomba. Anaomba katika Wafilipi 1:10–11 “ili mpate kutambua yale yaliyo mema; mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo, Mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu"
Comments