Vivuli na Vijito
- Dalvin Mwamakula
- Jul 31
- 2 min read

Utukufu wa Bwana na udumu milele; Bwana azifurahie kazi zake, yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, aigusaye milima nayo ikatoa moshi! Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote; Nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, ninapofurahi katika Bwana. (Zaburi 104:31-34)
Mungu hufurahia kazi za uumbaji kwa sababu zinatuelekeza zaidi kwa Mungu mwenyewe kuliko kwenye uumbaji wake.
Mungu anamaanisha tushangazwe na kustaajabishwa na kazi yake ya uumbaji. Lakini si kwa ajili yake yenyewe. Anamaanisha tuuangalie uumbaji wake na kusema: Ikiwa kazi tu ya vidole vyake (vidole vyake tu! Zaburi 8:3) imejaa hekima na nguvu na ukuu na adhama na uzuri, Mungu huyu atakuwaje yeye mwenyewe!
Hizi ni sehemu za nyuma za utukufu wake, kana kwamba zinaonekana katika giza kupitia kioo. Itakuwaje kuuona utukufu wa Muumba mwenyewe! Sio kazi zake tu! Mabilioni ya nyota hayatatosheleza nafsi ya mwanadamu. Mungu na Mungu pekee ndiye mwisho wa roho.
Jonathan Edwards aliielezea hivi:
Furaha ya Mungu ndiyo furaha pekee ambayo nafsi zetu zinaweza kuridhika nayo. Kwenda mbinguni na kumfurahia Mungu kikamilifu ni bora zaidi kuliko makazi mazuri zaidi hapa duniani. . . . [Haya] ni vivuli tu; lakini Mungu ndiye kiini. Hii ni miale iliyotawanyika tu; lakini Mungu ndiye jua. Hivi ni vijito tu; lakini Mungu ni bahari.
Hii ndiyo sababu Zaburi ya 104 inafikia tamati katika mistari ya 31-34 kwa kumlenga Mungu mwenyewe. “Nitamwimbia Mungu wangu nikiwa hai. . . . Kwa maana mimi nafurahi katika Bwana.”
Mwisho wa yote, haitakuwa bahari au milima au mabonde au buibui wa maji au mawingu au galaksi kubwa ambazo zitajaza mioyo yetu na mshangao na kujaza vinywa vyetu na sifa za milele. Itakuwa ni Mungu mwenyewe.




Comments