Wakati Wake Ni Mkamilifu
- Dalvin Mwamakula
- Jun 30
- 2 min read

Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate neema ya kutusaidia wakati ufaao. (Waebrania 4:16 , tafsiri halisi ya John Piper)
Najua mstari huu wa thamani kwa kawaida hutafsiriwa, “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Lakini hiyo ni tafsiri - ya kweli - ili kuonyesha kwamba Mungu hujitokeza mara tu wakati tunapomhitaji. Lakini lengo halisi ni jinsi msaada unavyokuja kwa wakati unaofaa.
Huduma yote iko katika siku zijazo - kwa muda mfupi, au mwezi mmoja, au mwaka, au muongo mmoja. Tuna muda wa kutosha wa wasiwasi juu ya upungufu wetu. Hili linapotokea, lazima tugeukie maombi.
Maombi ni aina ya imani inayotuunganisha leo na neema ambayo itatufanya tuwe na uwezo wa huduma ya kesho. Kuzigatia muda ni muhimu sana.
Je, inakuwaje kama neema imekuja mapema sana au imekuja kwa kuchelewa sana? Tafsiri ya kitamaduni ya Waebrania 4:16 haiweki wazi ahadi ya thamani sana katika suala hili. Tunahitaji tafsiri halisi zaidi ili kuiona. Ahadi sio tu kwamba tunapata neema ya "kusaidia wakati wa mahitaji," lakini kwamba neema imepangwa vizuri kwa wakati ufaao na Mungu.
Hoja ni kwamba maombi ndiyo njia ya kupata neema ya wakati ujao kwa msaada wa wakati unaofaa. Neema hii ya Mungu daima hufika kutoka "kiti cha neema" kwa wakati. Neno "kiti cha enzi cha neema" linamaanisha kwamba neema ya baadaye inatoka kwa Mfalme wa ulimwengu ambaye huweka nyakati kwa mamlaka yake mwenyewe (Matendo 1: 7).
Wakati wake ni mkamilifu, lakini si wakati wetu:
“Kwa maana miaka elfu machoni pake ni kama jana inapokuwa imepita” (Zaburi 90:4). Katika ngazi ya kimataifa, anaweka nyakati za mataifa kuinuka na kuanguka (Matendo 17:26). Na katika kiwango cha kibinafsi, "Nyakati zangu ziko mkononi mwake" (Zaburi 31:15).
Tunaposhangaa kuhusu wakati wa neema ya wakati ujao, ni lazima tufikiri juu ya "kiti cha ezni cha neema." Hakuna kinachoweza kuzuia mpango wa Mungu kutuma neema wakati itakuwa bora kwetu. Neema ya wakati ujao huja katika wakati ufaao.




Comments