top of page

Wanamapinduzi kwa Ajili ya Mwokozi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 1 min read
ree

Yesu alipokutana na mtu aliyekuwa na mapepo huko Gadara, mapepo yalipiga kelele, “Una nini nasi, Ee Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati?" (Mathayo 8:29)

 

Mapepo walijifunza siri hapa. Walijua kuwa wamehukumiwa. Walijua kwamba Mwana wa Mungu angekuwa mshindi. Lakini hawakujua hadi ilipotokea kwamba Kristo alikuwa anakuja kabla ya wakati wa kushindwa kwa mwisho. 

 

Kristo hatasubiri hadi mwisho wa vita kuongoza majeshi yake kwenda vitani. Ameanza kuongoza kikosi cha mapinduzi kwenda katika ardhi ya Shetani. Amefundisha "kikosi cha maisha” kufanya operesheni za uokoaji za uthubutu. Kristo amepanga ushindi mwingi wa kimkakati kabla ya wakati wa ushindi wa mwisho wa kimkakati.

 

Mtazamo wa vita unaotokana na hili ni huu: Kwakuwa kuangamia kwa Shetani ni hakika, na yeye anajua hivyo, tunaweza kumkumbusha kila wakati anapojaribu kutushawishi kumfuata. Tunaweza kucheka na kusema, “Umechanganyikiwa. Nani anataka kuungana na aliyeshindwa?!"

 

Kristo ameanzisha mapinduzi dhidi ya ufalme wa Shetani, na amewaita watu wake kuwa wanamapinduzi wa wokovu.

Kanisa ni adui aliyewekwa huru wa “mungu wa dunia hii” (2 Wakorintho 4:4). Sisi ni wapiganaji wa msituni na wadudu wanaokera. Sisi ni waasi dhidi ya ufalme wa uasi wa “mkuu wa nguvu za anga” (Waefeso 2:2). 

 

Sio salama. Lakini inasisimua. Maisha mengi yanapotezwa. Nguvu za Shetani daima zinatafuta shughuli zetu za uasi. Kristo amehakikisha ufufuo kwa wote wanaopigana hadi kifo. Lakini hajahakikisha faraja, au kukubalika na dunia, au ustawi katika eneo la adui. 

 

Wengi wamejitolea maisha yao kwa furaha nyuma ya mistari wa adui wakifanya kazi za Kamanda. Sioni njia bora ya kuishi — au kufa!

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page