Watu kwa ajili ya Jina Lake
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 2 min read
Updated: May 1

“Simeoni amesimulia jinsi Mungu alivyowajia Mataifa kwanza ili kupata kutoka kwao watu kwa ajili ya jina lake.” (Matendo 15:14)
Haiwezekani kusisitiza zaidi umuhimu wa jina la Mungu, yaani, umaarufu wa Mungu, katika kuhamasisha utume wa kanisa.
Petro alipogeuziwa ulimwengu wake juu chini kwa maono ya wanyama wachafu katika Matendo 10, na kwa somo kutoka kwa Mungu kwamba anapaswa kuwahubiria watu wa mataifa mengine pamoja na Wayahudi, alirudi Yerusalemu na kuwaambia mitume kwamba yote yalikuwa ni kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya jina lake. Tunajua hilo kwa sababu Yakobo alifupisha hotuba ya Petro hivi:
“Ndugu, nisikilizeni. Simeoni amekwesha kutueleza jinsi Mungu, kwa mara ya kwanza alivyoonyesha kuhusika kwa kujichagulia watu kutoka watu wa mataifa kwa ajili ya jina lake.” (Matendo 15:13–14).
Haishangazi kwamba Petro angesema kwamba kusudi la Mungu lilikuwa kukusanya watu kwa ajili ya jina lake; kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amemchoma Petro miaka kadhaa mapema kwa somo lisilosahaulika.
Unakumbuka kwamba, baada ya kijana mmoja tajiri kugeuka kutoka kwa Yesu na kukataa kumfuata, Petro alimwambia Yesu, “Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata wewe [tofauti na tajiri huyu]. Tutapata nini basi?” (Mathayo 19:27). Yesu alijibu kwa karipio la upole, ambalo kwa kweli lilisema kwamba hakuna dhabihu kubwa unapoishi kwa ajili ya jina la Mwana wa Adamu. Alisema, “Kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu au dada au baba au mama au watoto au mashamba kwa ajili ya jina langu atapokea mara mia na kuurithi uzima wa milele” (Mathayo 19:29).
Ukweli uko wazi: Mungu anafuatia kwa furaha kuu kusudi la ulimwenguni pote la kukusanya watu kwa ajili ya jina lake kutoka katika kila kabila na lugha na taifa (Ufunuo 5:9; 7:9). Ana shauku isiyoisha kwa ajili ya umaarufu wa jina lake kwa mataifa.
Kwa hiyo, tunapofanya mapenzi yetu yapatane na yake, na, kwa ajili ya jina lake, kukataa kutafuta umaarufu na starehe za kilimwengu, na kujiunga na kusudi lake la kimataifa, ahadi ya Mungu yenye uwezo wote kwa jina lake huruka kama bendera mbele yetu, na hatuwezi kupoteza, hata ikiwa ni lazima tutembee katika dhiki nyingi (Matendo 14:22; Warumi 8:35–39).




Comments