top of page

Wema Wetu Ni Furaha Ya Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 30
  • 1 min read
ree

“Nitafanya nao agano la milele, kwamba sitageuka na kuacha kuwatendea mema. Nami nitatia hofu yangu mioyoni mwao, ili wasinigeuke. Nitafurahi kuwatendea mema, nami nitawapanda katika nchi hii kwa uaminifu, kwa moyo wangu wote na kwa roho yangu yote.” (Yeremia 32:40-41)


Mungu kujitafutia sifa kutoka kwetu na sisi kujitafutia furaha ndani yake ni jitihada moja na ile ile.

Jitihada ya Mungu kutukuzwa na jitihada yetu ya kuridhika zinafikia lengo lao katika namna hii moja: furaha yetu ndani ya Mungu, ambayo ina miminika katika sifa.

 

Kwa Mungu, sifa ni mwangwi mzuri wa ubora wake katika mioyo ya watu wake. Kwetu sisi, sifa ni kilele cha kuridhika kinachotokana na kuishi katika ushirika na Mungu.

 

Maana ya kustaajabisha ya ugunduzi huu ni kwamba nguvu zote zenye uwezo wote zinazosukuma moyo wa Mungu kutafuta utukufu wake mwenyewe pia humsukuma kuridhisha mioyo ya wale wanaotafuta furaha yao ndani yake.

 

Habari njema za Biblia ni kwamba Mungu hakatai hata kidogo kutosheleza mioyo ya wale wanaomtumaini. Kinyume kabisa: Jambo lile lile linaloweza kutufanya tuwe na furaha zaidi ni lile ambalo Mungu hupendezwa nalo kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote. Hayo ni maneno ya ajabu: “Nitashangilia katika kuwatenda mema . . . kwa moyo wangu wote na kwa roho yangu yote” (Yeremia 32:41).

 

Kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, Mungu anaungana nasi katika kutafuta furaha yetu ya milele kwa sababu ukamilifu wa furaha hiyo ndani yake unarudi kuwa utukufu wa thamani yake isiyo na kikomo.

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page