top of page

Wote Wana Uadui na Mungu

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • May 29
  • 2 min read
ree

 Hapo kwanza mlikuwa mmetengana na Mungu, na mlikuwa adui zake katika nia zenu kwa sababu ya mienendo yenu mibaya. Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Kristo kupitia mauti. (Wakolosai 1:21–22)

 

Habari njema zaidi ulimwenguni pote ni kwamba kutengwa kwetu na Mungu kumekomeshwa na kupatanishwa na Hakimu wa ulimwengu wote mzima. Mungu hayuko kinyume chetu tena, bali yu kwa ajili yetu. Kuwa na upendo wa muweza wa yote upande wetu huimarisha sana roho. Maisha huwa huru kabisa na ya kuthubutu wakati kiumbe chenye nguvu zaidi katika ulimwengu ni kwa ajili yako.

 

Lakini ujumbe wa Paulo wa wokovu si habari njema kwa wale wanaokataa utambuzi katika Wakolosai 1:21.  Anasema, "mlikuwa mmetengwa na kuwa na uadui katika nia zenu." 

 

Je! ni watu wangapi unaowajua wanaosema, “Mbali na neema ya Mungu, mimi ni adui wa Mungu katika nia yangu”? Watu husema mara chache, “Mimi namchukia Mungu.” Kwa hiyo, Paulo anamaanisha nini kwamba watu wana “uadui katika nia zao” kwa Mungu kabla ya kupatanishwa na damu ya Kristo? 

 

Uhasama huo ni dhidi ya Mungu wa kweli, lakini watu humfikiria kwa namna wanavyomtaka awe na mara chache huzingatia uwezekano wa kuwa hatarini mbele yake.

Nadhani anamaanisha kwamba uhasama huo uko kweli dhidi ya Mungu wa kweli, lakini watu hawajiruhusu kumfikiria Mungu wa kweli. Badala yake, wanamwazia Mungu jinsi wanavyotamani awe, na mara chache sana huwa wanafikiria uwezekano kwamba huenda wako katika hatari kubwa mbele zake.

 

Lakini kuhusu Mungu ambaye yuko kweli kweli—Mungu ambaye ni mkuu juu ya vitu vyote, ikiwemo magonjwa na majanga—sote tulikuwa na uadui naye, Paulo asema. Moyoni, tulichukia nguvu na mamlaka yake kamili. 

 

Kwamba yeyote kati yetu ambaye ameokolewa ni mdeni kutokana na ukweli wa ajabu kwamba kifo cha Kristo kilitupatia neema ambayo Mungu alishinda mioyo yetu na kutufanya tumpende Yule tuliyemchukia hapo awali. 

 

Wengi bado wanajifunza kutokuwa na uadui na Mungu. Ni jambo jema kuwa ana subira iliyotukuka.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page