top of page

Yesu Anatuombea

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Nov 14
  • 1 min read
ree

Aweza kuwaokoa kabisa wale wanaomkaribia Mungu kwa yeye, kwa kuwa yu hai siku zote ili kuwaombea. (Waebrania 7:25)

 

Inasema kwamba Kristo anaweza kuokoa hadi mwisho - milele - kwa kuwa yeye anaishi daima ili kufanya maombezi kwa ajili yetu. Kwa maneno mengine, hasingeweza kutuokoa milele ikiwa hasingeendelea kutuombea milele.

 

Hii ina maana kwamba wokovu wetu ni salama kama vile ukuhani wa Kristo usioharibika. Hii ndiyo sababu tulihitaji kuhani mkuu kuliko kuhani yeyote wa kibinadamu. Uungu wa Kristo na kufufuka kwake kutoka kwa wafu kunahakikisha ukuhani wake usioharibika kwa ajili yetu.

 

Hii ina maana kwamba hatupaswi kuzungumza juu ya wokovu wetu kwa maneno tuli jinsi tunavyofanya mara nyingi - kana kwamba nilifanya jambo mara moja katika tendo la uamuzi, na Kristo alifanya kitu mara moja alipokufa na kufufuka tena, na hiyo ndiyo yote. Hayo sio jumla ya yote yaliyo kwenye jambo hili. 

 

Siku hii hii ninaokolewa kwa maombezi ya milele ya Yesu mbinguni. Yesu anatuombea na hilo ni muhimu kwa wokovu wetu.

 

Tunaokolewa milele kwa maombi ya milele (Warumi 8:34) na utetezi (1 Yohana 2:1) wa Yesu mbinguni kama Kuhani wetu Mkuu. Anatuombea na maombi yake yanajibiwa kwa sababu anaomba kikamilifu kwa msingi wa dhabihu yake kamilifu.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page