top of page

Yesu Atamaliza Kazi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Feb 26
  • 2 min read
ree

"Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote, halafu mwisho utakuja." (Mathayo 24:14)

 

Sijui ahadi nyingine yoyote ya kimishonari inayotia moyo zaidi kuliko neno hili kutoka kwa Yesu.

Sio: Injili hii inapaswa kuhubiriwa. Sio: Injili hii inaweza kuhubiriwa. Lakini: Injili hii itahubiriwa.

Hili sio agizo kuu, wala amri kuu. Ni uhakika mkubwa, ujasiri mkubwa.


Nani anaweza kuthubutu kuzungumza hivyo? Anajuaje kuwa itakuwa hivyo? Anawezaje kuwa na uhakika kwamba kanisa halitashindwa katika kazi yake ya umishonari?


Jibu: Neema ya huduma ya umishonari haizuiliki kama neema ya kuzaliwa upya. Kristo anaweza kuahidi kutangazwa kwa ulimwengu wote kwa sababu yeye ni mkuu. Anajua mafanikio ya baadaye ya misheni kwa sababu yeye ndiye anaye tengeneza siku zijazo. Mataifa yote yatasikia!


Misheni haiwezi kushindwa, kwa maana Kristo, anayetengeneza siku zijazo, ameahidi: ‘Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote.

"Taifa" sio nchi ya "kisasa". Agano la Kale liliposema kuhusu mataifa, lilimaanisha makundi kama Wajebusi, Waperizi, Wahivi, Waamori, Wamoabi, Wakanaani, na Wafilisti. "Mataifa" ni makundi ya kikabila yenye lugha na utamaduni wao maalum. Zaburi 117:1: "Msifuni Bwana, enyi mataifa yote! Msifuni, enyi watu wote! Mataifa ni watu — makundi ya watu, kama tunavyoyaita.


Kama Mwana wa Mungu mwenye enzi na Bwana wa kanisa, Yesu alichukua tu kusudi hili la kimungu na kusema kwa uhakika kamili, “Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote” (Mathayo 24:14).


Sababu ya misheni za dunia zina uhakika kabisa wa mafanikio. Hauwezi kushindwa. Je, si jambo la busara basi kwamba tuombe kwa imani kuu, kwamba tuweze kuwekeza kwa ujasiri mkubwa, na kwamba twende tukiwa na hisia za ushindi wa uhakika?

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page