Yesu Atawakanyaga Maadui Zetu Wote
- Dalvin Mwamakula
- Jul 31
- 1 min read

Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. (1 Wakorintho 15:24)
Utawala wa Kristo unaenea kwa umbali gani?
Mstari unaofuata, 1 Wakorintho 15:25 unasema, “Lazima atawale mpaka atakapowaweka adui zake wote chini ya miguu yake.” Neno wote linatuambia kiwango.
Ndivyo linavyofanya neno kila katika mstari wa 24: “Hapo ndipo mwisho, atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu.”
Hakuna ugonjwa, hakuna uraibu, hakuna pepo, hakuna tabia mbaya, hakuna kosa, hakuna uovu, hakuna udhaifu, hakuna hasira, hakuna hisia, hakuna kiburi, hakuna kujihurumia, hakuna ugomvi, hakuna wivu, hakuna upotovu, hakuna choyo, hakuna uvivu ambao Kristo hataushinda kama adui wa heshima yake.
Na faraja katika ahadi hiyo ni kwamba unapojitayarisha kupambana na maadui wa imani yako na utakatifu wako, hutapigana peke yako.
Yesu Kristo sasa, katika ulimwengu huu, anawaweka adui zake wote chini ya miguu yake. Kila utawala na kila mamlaka na kila nguvu itashindwa.
Kwa hiyo, kumbuka kwamba kiwango cha utawala wa Kristo kinamfikia kila adui mdogo na mkubwa wa utukufu wake katika maisha yako, na katika ulimwengu huu. Atashindwa.




Comments