Yesu na Utafutaji wa Furaha
- Dalvin Mwamakula
- Sep 2
- 2 min read

[Mtazameni] Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, na ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. (Waebrania 12:2)
Je, mfano wa Yesu unapingana na kanuni ya Furaha ya Kikristo ? Kwamba, upendo ni njia ya furaha na mtu anapaswa kuuchagua kwa sababu hiyo, ili asionekane akifanya utii kwa Mungu kwa shingo upande au kuchukizwa na fursa ya kuwa chombo cha neema au kudharau thawabu iliyohadiwa.
Waebrania 12:2 inaonekana kusema kwa uwazi kabisa kwamba Yesu hakupinga kanuni hii.
Kazi kubwa zaidi ya upendo iliyowahi kutokea iliwezekana kwa sababu Yesu alitafuta furaha kubwa zaidi inayoweza kufikiriwa, yaani, furaha ya kutukuzwa mkono wa kuume wa Mungu katika kusanyiko la watu waliokombolewa: “Kwa furaha iliyowekwa mbele yake [yeye] alivumilia msalaba!”
Kazi kubwa ya upendo ilifanikishwa kwa sababu Yesu alitafuta furaha kuu zaidi: kutukuzwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu katika kusanyiko la waliokombolewa.
Kwa kusema hivi, mwandishi anamaanisha kumpa Yesu kama mfano mwingine, pamoja na watakatifu wa Waebrania 11, wa wale ambao wana hamu kubwa na wana uhakika katika furaha ambayo Mungu anatoa kiasi kwamba wanakataa “anasa za dhambi za muda mfupi” (Waebrania 11:25) na kuchagua kuteseka ili waweze kwenda sawa na mapenzi ya Mungu.
Kwa hiyo, si kinyume na Biblia kusema kwamba angalau sehemu ya kile kilichomsaidia Kristo katika saa za giza za Gethsemane ilikuwa tumaini la furaha baada ya msalaba. Hii haipunguzi ukweli na ukuu wa upendo wake kwetu, kwa sababu furaha ambayo aliitarajia ilikuwa furaha ya kuwaongoza wana wengi kwenye utukufu (Waebrania 2:10).
Furaha yake iko katika ukombozi wetu, ambao unaongezeka kwa utukufu wa Mungu. Tunashiriki furaha na Yesu na Mungu anapata utukufu.




Comments