top of page

Yesu Ndiye Unayemtafuta

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Jul 31
  • 2 min read
ree

Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,  nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa dahari.”  (Mathayo 28:18-20)

 

Sura ya mwisho ya Mathayo ni dirisha linalofunguka kuelekea mawio ya utukufu wa Kristo aliyefufuka. Kupitia hilo unaweza kuona angalau vilele vitatu vikubwa katika safu ya milima ya tabia ya Kristo: kilele cha uwezo wake; kilele cha fadhili zake; na kilele cha makusudi yake. 

 

Mamlaka yote ni yake - haki na uwezo wa kufanya mapenzi yake. Naye anatumia uwezo huo ili kutimiza kusudi lake lisiloyumbayumba la kufanya wanafunzi kutoka kwa mataifa yote. Na katika mchakato huo yeye ni mwenye fadhili kwetu kibinafsi, akiahidi kuwa nasi hadi mwisho.

 

Sote tunajua mioyoni mwetu kwamba ikiwa Kristo aliyefufuka atatutosheleza shauku zetu kutamani ukuu, hivyo ndivyo namna anapasa kuwa. Mkuu katika nguvu. Mkuu katika wema. Mkuu katika kuwa na makusudi.

 

Watu ambao ni dhaifu sana kutimiza malengo yao hawawezi kutosheleza tamaa yetu ya kuvutiwa na ukuu. Hatuvutiwi hata kidogo na watu ambao hawana kusudi maishani. Na hata kidogo zaidi na wale ambao malengo yao ni ya ubinafsi na yasiyo na huruma. 

 

Tunachotamani kuona na kujua ni Mtu ambaye nguvu zake hazina kikomo, ambaye fadhili zake ni mwanana, na ambaye kusudi lake ni moja na lisiloyumba. 

 

Waandishi wa riwaya na washairi na watengenezaji filamu na waandishi wa TV mara kwa mara huunda kivuli cha Mtu huyu. Lakini hawawezi kutosheleza shauku yetu ya kuabudu kama vile  jarida la 'National Geographic' la mwezi huu haliwezi kutosheleza shauku yangu ya kuiona 'Grand Canyon'.

 

Lazima tuwe na kitu halisi. Lazima tuone Asili ya nguvu zote na wema wote na kusudi zote. Ni lazima tumwone na kumwabudu Kristo aliyefufuka.

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page