top of page

Zawadi ya Mungu Isiyoelezeka

  • Writer: Joshua Phabian
    Joshua Phabian
  • 9 hours ago
  • 2 min read
ree

Ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa kifo cha Mwana wake, zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa kwa uzima wake. Zaidi ya hayo, sisi pia tunafurahi katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumepata upatanisho. (Warumi 5:10-11)


Je, tunapokeaje upatanisho na shangwe katika Mungu? Tunafanya hivyo kupitia Yesu Kristo. Inayomaanisha, angalau, kwamba tunafanya taswira ya Yesu katika Biblia - yaani, kazi na maneno ya Yesu yanayoonyeshwa katika Agano Jipya - tunaifanya taswira hiyo kuwa maudhui muhimu ya furaha yetu juu ya Mungu. Kushangilia katika Mungu bila maudhui ya Kristo hakumheshimu Kristo. Na pale Kristo asipoheshimiwa, Mungu haheshimiwi.


Kwa maana tulipokuwa tungali dhaifu, wakati ufaao Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.

Katika 2 Wakorintho 4:4–6, Paulo anaelezea wongofu kwa njia mbili. Katika mstari wa 4, anasema ni kuona “utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.” Na katika mstari wa 6, anasema ni kuona “utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.” Kwa vyovyote vile unaiona hoja.. Tunaye Kristo, sura ya Mungu, na tunaye Mungu katika uso wa Kristo.


Ili kushangilia katika Mungu, tunashangilia katika kile tunachoona na kujua juu ya Mungu katika mfano wa Yesu Kristo. Na hii inakuja kwa uzoefu wake kamili wakati upendo wa Mungu unamiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu, kama Warumi 5:5 inavyosema. Na uzoefu huo mtamu, uliotolewa na Roho wa upendo wa Mungu unapatanishwa nasi tunapotafakari ukweli wa kihistoria wa mstari wa 6, “Kwa maana tulipokuwa tungali dhaifu, wakati ufaao Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.”


Kwa hivyo hapa ndio jambo la Krismasi. Mungu hakununua tu upatanisho wetu kwa kifo cha Bwana Yesu Kristo (Warumi 5:10), na sio tu kwamba Mungu alituwezesha kuupokea upatanisho huo kwa njia ya Bwana Yesu Kristo, bali hata sasa tunafurahi katika Mungu mwenyewe kwa njia ya Kristo. Roho, kwa Bwana wetu Yesu Kristo (Warumi 5:11).


Yesu alinunua upatanisho wetu. Yesu alituwezesha kupokea upatanisho na kufungua zawadi. Na Yesu mwenyewe anang'aa kama zawadi isiyoelezeka - Mungu katika mwili - na kuchochea shangwe yetu yote katika Mungu.


Mtazame Yesu Krismasi hii. Pokea upatanisho alionunua. Usiweke zawadi kwenye rafu bila kufunguliwa. Na unapoifungua, kumbuka Mungu mwenyewe ni zawadi ya upatanisho na Mungu.


Furahi ndani yake. Mjue kama furaha yako. Mjue kama hazina yako.







Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page