top of page

Ziara Iliyokuwa Inasubiriwa Kwa Muda Mrefu

  • Writer: Joshua Phabian
    Joshua Phabian
  • Dec 4
  • 1 min read

Updated: Dec 5

ree

“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa. Naye amtusimamishia penbe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi wake, kama alivyonena kwa vinywa vya manabi wake watakatifu tanguzamani, kwamba atatuokoa kutoka kwa   adui zetu na kutoka mikononi mwa wote watuchukiao.” (Luka 1:68-71)

 

Angalia mambo mawili ya ajabu kutoka kwa maneno haya ya Zekaria, mume wa Elisabeti, katika Luka 1.

 

Kwanza, miezi tisa mapema, Zekaria hakuamini kwamba mke wake angelipata mtoto. Sasa, akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu, ana uhakika sana na kazi ya Mungu ya ukombozi katika Masihi ajaye hivi kwamba anaiweka katika wakati uliopita: “amewajia na kuwakomboa watu wake.” Kwa akili ya imani, tendo lililoahidiwa la Mungu ni sawa na limefanywa. Zekaria amejifunza kumkubali Mungu kwa neno lake na hivyo ana uhakikisho wa ajabu: Mungu “ametembelea na kukomboa!” (Luka 1:68).

 

Kwa akili ya imani, tendo lililoahidiwa la Mungu ni sawa na limefanywa.

Pili, kuja kwa Yesu Masihi ni kutembelewa na Mungu kwa ulimwengu wetu: Mungu wa Israeli ametembelea na kukomboa. Kwa karne nyingi, watu wa Kiyahudi walikuwa wamedhoofika chini ya usadikisho kwamba Mungu alikuwa amejiondoa: roho ya unabii ilikuwa imekoma; Israeli ilikuwa imeanguka mikononi mwa Rumi. Na wacha Mungu wote katika Israeli walikuwa wakingojea kujiliwa na Mungu. Luka anatuambia kwamba mzee mwingine, Simeoni mcha Mungu, alikuwa "akingojea faraja ya Israeli" (Luka 2:25). Vivyo hivyo, Ana mwenye maombi alikuwa "akingojea ukombozi wa Yerusalemu" (Luka 2:38).

 

Hizi zilikuwa siku za matarajio makubwa. Sasa ujio wa Mungu uliokuwa ukingojewa kwa muda mrefu ulikuwa karibu kutokea - hakika, alikuwa karibu kuja kwa njia ambayo hakuna mtu aliyetarajia.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page