top of page

Fanya Vita na Kutokuamini

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Sep 2
  • 2 min read
ree

Katika hali zote itwaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mwaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu; na ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. (Waefeso 6:16-17)


Wakati ninapokuwa na wasiwasi kuhusu kuzeeka, napambana na kutoamini kwa ahadi, "Hata katika uzee wako mimi ni yeye, na hadi nywele zako za kijivu nitakubeba. Mimi nimefanya, nami nitashikilia; nitabeba na kuokoa” (Isaya 46:4).

 

Ninapokuwa na wasiwasi juu ya kufa, ninapambana na kutoamini kwa ahadi kwamba “hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe, na hakuna hata mmoja wetu anayekufa kwa ajili yake mwenyewe. Kwa maana tukiishi, twaishi kwa Bwana, na tukifa, twafa kwa Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni wa Bwana. Kwa maana Kristo alikufa kwa ajili hiyo, akaishi tena, ili wapate kuwa Bwana wa waliokufa na walio hai pia” (Warumi 14:7–9).

 

Kutokuamini ahadi za Mungu ni mzizi wa wasiwasi, ambao, kwa upande wake, ni mzizi wa dhambi nyingine nyingi.

Ninapokuwa na wasiwasi ili nivunjike imani na kungunguka kutoka kwa Mungu, ninapambana na kutokuamini kwa ahadi, “Yeye aliyeanza kazi njema ndani yenu ataimaliza hata siku ya Yesu Kristo” (Wafilipi 1:6); na, “Aweza kuwaokoa kabisa wao wamkaribiao Mungu kwa yeye, maana yu hai siku zote ili kuwaombea” (Waebrania 7:25).

 

Jiunge nami katika vita hii! Tufanye vita, si na watu wengine, bali na kutokuamini kwetu wenyewe. Kutokuamini ahadi za Mungu ni mzizi wa wasiwasi, ambao, kwa upande wake, ni mzizi wa dhambi nyingine nyingi. Upanga wa Roho ni neno la Mungu, Paulo alisema katika Waefeso 6:17. Ngao ambayo kwayo tunazima hila za moto za Shetani ni imani (mstari wa 16) - imani katika neno hilo hilo la Mungu. Basi shika ngao katika mkono wako wa kushoto na upanga katika mkono wako wa kulia, na tupige vile vita vizuri vya imani.

 

Chukua Biblia, mwombe Roho Mtakatifu akusaidie, weka ahadi moyoni mwako, na pigana vita vilivyo vizuri— kuishi kwa imani katika neema ya wakati ujao.

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page