Imani Halisi Dhidi ya Imani Ya Udanganyifu
- Dalvin Mwamakula
- Apr 28
- 1 min read
Updated: May 1

Kristo, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi, atatokea mara ya pili, sio kushughulikia dhambi, bali kuwaokoa wale wanaomngoja kwa hamu. (Waebrania 9:28)
Swali lililo mbele yetu sote ni: Je, tunajumuishwa katika “wengi” ambao Kristo alibeba dhambi zao? Na je, tutaokolewa katika kuja kwake mara ya pili?
Jibu la Waebrania 9:28 ni, “Ndiyo,” ikiwa ‘tunamngoja yeye kwa hamu. Tunaweza kujua kwamba dhambi zetu zimeondolewa na kwamba tutakuwa salama katika hukumu, ikiwa tunamwamini Kristo kwa njia ambayo inatufanya tuwe na hamu ya kuja kwake.
Kuna imani ya udanganyifu inayodai kumwamini Kristo, lakini ni sera ya bima ya moto tu. Imani ya udanganyifu "huamini" ili kuepuka jehanam tu. Haina hamu ya kweli kwa ajili ya Kristo. Kwa kweli, ingependelea ikiwa asingelikuja, ili tuwe na raha nyingi za ulimwengu huu kadiri tuwezavyo. Hii inaonyesha kwamba moyo hauko pamoja na Kristo, bali pamoja na ulimwengu.
Kwa hiyo, suala kwetu ni:
Je, tunatamani kwa hamu kuja kwa Kristo? Au tunataka akae mbali, huku penzi letu na ulimwengu likiendelea?
Hilo ndilo swali linalojaribu uhalisia wa imani.
Acheni tuwe kama Wakorintho tunapo “subiria kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo” (1 Wakorintho 1:7), na kama Wafilipi ambao “uraia wao uko mbinguni, na kutoka humo tunamsubiria Mwokozi, Bwana Yesu Kristo. ” (Wafilipi 3:20).
Hilo ndilo suala kwetu. Je, tunapenda kufunuliwa kwake? Au je, tunaupenda ulimwengu na kutumaini kwamba kutokea kwake hakutokatisha mipango yetu? Umilele hutegemea swali hili.
コメント