Mafanikio Ya Dakika Za Mwisho
- Dalvin Mwamakula
- Jan 27
- 2 min read

"Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako." (Luka 23:42)
Moja ya wauaji wakubwa wa matumaini ni kwamba umejaribu kwa muda mrefu kubadilika, na haujafanikiwa.
Unatazama nyuma na kufikiria: Kuna faida gani? Hata kama ningeweza kupata mafanikio, kungekuwa na wakati mdogo sana wa kuishi katika njia yangu mpya ambayo haingeweza kuleta tofauti kubwa ikilinganishwa na miaka mingi ya kushindwa.
Yule mnyang'anyi wa zamani (mwizi msalabani karibu na Yesu) aliishi kwa saa nyingine au zaidi baada ya kuongoka kwake. Kisha akafa. Alibadilishwa. Aliishi msalabani kama mtu mpya mwenye mitazamo na matendo mapya (hakuna matukano tena). Lakini 99.99% ya maisha yake yalipotea. Je, masaa machache ya mwisho ya maisha mapya yalifaa?
Yalikuwa muhimu sana pasina kifani. Mnyang'anyi huyu wa zamani, kama sisi sote, atasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo kutoa hesabu ya maisha yake. “Imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kwamba ni mema au mabaya” (2 Wakorintho 5:10). Maisha yake yatashuhudiaje katika siku hiyo kuzaliwa kwake upya na muungano wake na Kristo? Je, maisha yake yatathibitishaje upya wake ndani ya Kristo?
Jipe moyo, mpiganaji. Endelea kuuliza, kutafuta, na kumwangalia Kristo. Mungu ana makusudi kwa kuchelewesha mafanikio yako.
Saa za mwisho zitasimulia hadithi. Mtu huyu alikuwa mpya. Imani yake ilikuwa ya kweli. Hakika ameunganishwa na Kristo. Haki ya Kristo ni yake. Dhambi zake zimesamehewa.
Hivyo ndivyo saa za mwisho zitakavyotangaza katika hukumu ya mwisho. Amebadilishwa! Na kubadilika kwake ni muhimu. Ilikuwa, na itakuwa, ushuhuda mzuri wa nguvu ya neema ya Mungu na ukweli wa imani yake na muungano wake na Kristo.
Sasa turudi kwenye mapambano yetu dhidi ya mabadiliko. Sisemi kwamba waumini wanaohangaika hawajaokolewa kama yule mnyang'anyi. Ninasema tu kwamba miaka ya mwisho na masaa ya mwisho ya maisha ni muhimu.
Ikiwa katika 1% ya mwisho ya maisha yetu, tunaweza kupata ushindi juu ya tabia fulani ya dhambi ya muda mrefu au kasoro yenye kuumiza katika utu wetu, itakuwa ni ushuhuda mzuri sasa wa nguvu ya neema; na itakuwa ushuhuda wa ziada (sio pekee) katika hukumu ya mwisho kwa imani yetu katika Kristo na muungano wetu naye.
Jipe moyo, mpiganaji. Endelea kuuliza, kutafuta, kubisha hodi. Endelea kumwangalia Kristo. Ikiwa Mungu anapata utukufu kwa kuokoa wanyang'anyi katika saa ya mwisho, hakika ana makusudi yake kwa nini amesubiri mpaka sasa ili kukupa mafanikio uliyoyatafuta kwa miaka mingi.




Comments