Mungu Si Mnyonge
- Dalvin Mwamakula
- Sep 30
- 2 min read

Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa; hubatilisha mipango ya mataifa. Shauri la Bwana lasimama milele, Mawazo ya moyo wake vizazi hata vizazi. (Zaburi 33:10-11)
“Mungu wetu yuko mbinguni; anafanya yote ayapendayo” (Zaburi 115:3). Maana ya andiko hili ni kwamba Mungu ana haki na uwezo wa kufanya lolote linalomfurahisha. Hiyo ndiyo maana ya kusema kwamba Mungu ni mwenye enzi kuu.
Fikiria jambo hilo kwa muda: Ikiwa Mungu ni mwenye enzi kuu na anaweza kufanya lolote analolipenda, basi hakuna kusudi lake lolote linaloweza kuzuiliwa. “BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa; hubatilisha mipango ya mataifa. Shauri la Bwana lasimama milele, mipango ya moyo wake vizazi hata vizazi” (Zaburi 33:10–11).
Na ikiwa hakuna madhumuni yake yoyote yanayoweza kuzuiliwa, basi lazima awe ndiye mwenye furaha kuliko viumbe vyote.
Furaha hii isiyo na kipimo na ya kimungu ni chemchemi ambayo Mkristo (Mwenye Furaha) hunywa na anatamani kunywa kwa kina zaidi.
Lengo letu ni kutumainia upendo wake thabiti. Kumkimbilia. Kumfurahia Mungu, kumthamini, na kufurahia ushirika na kibali chake.
Je, unaweza kuwazia jinsi ingekuwa ikiwa Mungu anayetawala ulimwengu hasingelikuwa na furaha?
Je, ingekuwaje kama Mungu angekuwa na tabia ya kunung’unika, kukasirika, na kuwa na huzuni, kama yule jitu katika hadithi ya Jack na Mharagwe wa Ajabu angani? Je, ingekuwaje kama Mungu angekuwa na hasira, udhaifu, huzuni kuu, kutoridhika, na kukata tamaa?
Je, tungeweza kuungana na Daudi na kusema, “Ee Mungu, wewe ndiwe Mungu wangu; nakutafuta kwa bidii; nafsi yangu ina kiu kwa ajili yako; mwili wangu unakuzimia kwa ajili yako, kama katika nchi kavu na uchovu, isiyo na maji” ( Zaburi 63:1 )? Sidhani.
Sote tungekuwa na uhusiano na Mungu kama watoto wadogo ambao wana baba aliyefadhaika, mwenye huzuni na asiyeridhika. Hawawezi kumfurahia. Wanaweza tu kujaribu kutomsumbua, au labda kujaribu kumfanyia kazi ili kupata kibali kidogo.
Lakini hivyo sivyo Mungu alivyo. Yeye kamwe hana hali mbaya ya hasira au kukata tamaa. Na, kama Zaburi 147:11 inavyosema, yeye “hujifurahisha . . . katika wale wanaotumainia fadhili zake. Lengo la Mhedonisti Mkristo si kumkwepa Mungu huyu, si kumkimbia, wala kutembea kwa tahadhari sebuleni ili huzuni yake isigeuke kuwa hasira. Hapana, lengo letu ni kutumainia upendo wake thabiti. Kumkimbilia. Kumfurahia Mungu, kumthamini na kufurahia ushirika na kibali chake.




Comments