Nguvu ya Ahadi Iliyokuu
- Dalvin Mwamakula
- Sep 2
- 2 min read

Nitatembea kwa uhuru, kwa maana nimetafuta mausia yako. (Zaburi 119:45, tafsiri yangu)
Kipengele muhimu cha furaha ni uhuru. Hakuna hata mmoja wetu ambaye angelifurahi ikiwa hatungelikuwa huru kutoka kwa kile tunachochukia na kuwa huru kwa kile tunachopenda.
Na tunapata wapi uhuru wa kweli? Zaburi 119:45 inasema, “Nitakwenda katika uhuru, kwa maana nimeyatafuta mausia yako.”
Picha inaonyesha maeneo ya wazi. Neno hutuweka huru kutoka katika udogo wa akili. “Mungu alimpa Sulemani . . . upana wa akili kama mchanga wa ufukwe wa bahari” (1 Wafalme 4:29). Neno hutuweka huru kutoka katika vifungo vya kutisha. “Akanitoa akanipeleka panapo nafasi” (Zaburi 18:19).
Yesu anasema, “Mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Uhuru alionao akilini ni uhuru kutoka katika utumwa wa dhambi (Yohana 8:34). Au, ili kuiweka vyema, ni uhuru kwa ajili ya utakatifu.
Ahadi za neema ya Mungu zinatoa nguvu zinazofanya matakwa ya utakatifu wa Mungu kuwa uzoefu wa uhuru badala ya hofu na kifungo.
Petro alieleza jinsi ahadi za Mungu zinavyoweza kuweka huru: “Kupitia [ahadi zake zenye thamani na kuu sana] mmekuwa washirika wa tabia ya kimungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2 Petro 1:4)).
Kwa maneno mengine, tunapoamini ahadi za Mungu, tunakata mzizi wa ufisadi na tamaa ya dhambi kwa nguvu ya ahadi kuu.
Neno linalovunja nguvu za anasa za uongo ni la muhimu kiasi gani! Na ni kwa uangalifu wa namna gani tunapaswa kuangaza njia zetu na kujaza mioyo yetu kwa Neno la Mungu!
"Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu" (Zaburi 119:105). “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi” (Zaburi 119:11).




Comments