top of page

Mkasa wa Furaha ya Dunia

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 3
  • 7 min read


Makala imeandwika na Tony Reinke

Mwandishi mkuu, desiringGod.org


Katika kitabu chake cha maarufu kiitwacho Mere Christianity , CS Lewis anatoa ufahamu wa kina katika injini ya kisaikolojia inayovuta maigizo ya historia. "Yote tunayoita historia ya mwanadamu - pesa, umaskini, tamaa, vita, ukahaba, madaraja, milki, utumwa - ni hadithi ndefu ya kutisha ya mwanadamu kujaribu kutafuta kitu kingine isipokuwa Mungu ambacho kitamfurahisha."


Ndiyo. Au kusema hili kimsingi zaidi: nia na misukumo inayoongoza katika historia ni matamanio ya furaha. Fikiria kuhusu hili, kila kitu kuanzia utumwa hadi ukahaba, ubaguzi wa rangi hadi ugaidi, unyang'anyi hadi utoaji mimba hadi uanzishaji wa vita vya dunia - yote yanaendeshwa na tamaa ya kuitafuta furaha mbali na Mungu.


Lewis anatoa hoja ya msingi kwa wanaomkana Mungu. Tatizo kubwa la kumkana Mungu sio kule kumkana Mungu kiakili, yaani kukana uwepo wa Mungu kabisa. Tatizo halisi ni kumkana Mungu kihisia, kuona Mungu kuwa kizuizi katika njia ya kutafuta furaha ya kibinafsi. Ukanaji Mungu huu wa kivitendo ndio mzizi wa tatizo la ubinadamu na unasumbua mioyo ya wanaomkana Mungu, wasioamini kwamba Mungu yupo na hata wanaodai kuwa wanaamini katika Mungu mmoja.


Tunatamani raha kama ngono, mamlaka, mali, na umaarufu, lakini hatuzipati. Tunatumia na kutumiwa, tukikataa vitu vya kuridhisha tunavyopewa na Mungu.

Wanaomkana Mungu mpaka kwenye kiini.

Saratani kama hiyo ndani ya moyo inaweza tu kuleta athari kubwa za kijamii. Kwa kugeuka kutoka kwa Mungu, ufuatiliaji wetu wa furaha isiyo ya Mungu lazima uje kwa gharama ya wengine (Zaburi 14: 1-4). Tatizo si kwamba kuna watu wanaomkana Mungu duniani; tatizo ni kwamba sisi sote tunajitambulisha ulimwenguni kote na ukanaji wa Mungu wa namna hii katika kiini cha nia zetu. Kila mmoja wetu amezaliwa na tamaa iliyopotoka ya furaha, na tamaa hiyo lazima iwagharimu wengine.


Kwa hivyo ni nini kinachotokea tunapotafuta furaha na lazima tumtumie mtu fulani kuipata? Lazima ufanye uonevu. Lazima ukanyage watu vidole. Lazima ujeruhi na kuudhi wengine. Na unakutana ana kwa ana na macho kwa macho na watu wengine wanaomkana Mungu wakitafuta furaha ya kibinafsi kwa gharama yako. Unatumiwa. Kwa kushangaza, tamaa hizi hutuvuta sisi kwa sisi, na kufanya athari kuwa ngumu zaidi, kama vile mgongano wa uso kwa uso usiozuilika kati ya treni za mizigo.


Mwanaume mseja ambaye huabudu sana ngono anahamasihwa kuchumbia kwa ajili msukumo huo. Mwanamke mseja ambaye huabudu umakini wa kuonekana kwa wanaume ili kufadhili hali yake ya kujistahi pia anahamasishwa kuchumbiwa. Wakikutana watatumiana kwa maslahi yao binafsi. Itamgharimu mwanaume kubembeleza, itamgharimu mwanamke mwili wake, lakini kwa wakati huu zitaonekana kuwa gharama ndogo kuridhisha sanamu zao za kibinafsi. Mpaka sasa kila kitu kinaonekana kuwa na amani.


Lakini sanamu hizi haziwezi kutosheka.. Hatimaye macho ya mwanaume yanavutwa kwa miili mingine ya wanawake wengine na kutovutiwa na mwanamke anayeketi kando ya meza hivi sasa. Ubembelezi huo hatimaye utafichuliwa kuwa ni ulaghai, na mwili wa mwanamke utaonyeshwa kuwa ulikuwa tu kitu cha tamaa ya mwanamume. Ukitazama ndani zaidi, unakuta katika uhusiano huu wenye dhambi wawili waliojitenga, wamkanao Mungu ambao mapenzi yao yametenganishwa na Mungu, na wanaotumiana wao kwa wao kujaza pengo. Itaishia kwa vita.


Klabu ya Kupambana


"Katika mizizi, dhambi sio tu kufanya makosa, ni kuabudu makosa."

Kutumiana kwa lengo la furaha ya kibinafsi, ingawa inaonekana kwa hila, hatimaye hupelekea mgogoro mbaya wa kibinafsi katika maisha yetu wote. Yakobo 4:1–12 inatusaidia kuelewa ni kwanini hii inatokea kwa kutuuliza wazi: Ni nini husababisha mapigano na ugomvi maishani mwetu? Ni nini kinachochochea moto wa hasira, uchungu, na ghadhabu unayohisi moyoni mwako?

Jibu si gumu. Tunapigana sisi kwa sisi kwa sababu ya tamaa zetu hulilia furaha zisizo na Mungu.


Tunatamani raha tunazofikiri zitatuletea furaha, lakini hatuwezi kuzikidhi tamaa hizo. Kwa hivyo tunaua. Tunatamani na kuabudu raha tunayofikiri itaridhisha nafsi zetu - ngono, mamlaka, mali, umaarufu, we taja yoyote - lakini hatuzipati, zinabaki kuwa mbali mikononi mwetu, na kwa hivyo tunauana. Tunatumia. Tunatumiwa. Tunatamani. Tunakuwa maadui sisi kwa sisi. Tunakuwa maadui wa Mungu. Tunakataa vitu vingi ambavyo Mungu anatupatia vya kuturidhisha. Karibu kwenye klabu ya mapambano.


Puritan Richard Sibbes aeleza sababu rahisi inayofanya hayo yote kuwa ya kweli: “Kabla ya moyo kubadilishwa, hukumu yetu inapotoka kuhusiana na mwisho wetu; tunatafuta furaha yetu mahali ambapo haipatikani.” Katika maisha yetu, hili ndilo mzizi wa tatizo nyuma ya migogoro. Sisi ni vipofu kwa kile kitakacholetea mioyo yetu utoshelevu inaoutamani. Hatuwezi kuona uzuri wa Mungu au kufurahia mazuri ya Mungu, kwa hiyo tunatafuta mibadala ya anasa za mwili. Mioyo yetu imerudi nyuma sana imekufa. Tunaishia kufukuzia mwisho mbaya wa mwisho mbaya.


Lakini sote tunatafuta kitu. Hiyo ndiyo hoja ya Lewis.

Kwa hivyo "mwisho" ni nini? "mwisho wangu " ni upi? Mpuritani Richard Baxter anaeleza. Mwisho wetu ni furaha yetu, hazina yetu, wema wetu mkuu, kile tunachotumia kila kitu katika maisha yetu kukipata. "Mwisho" wetu ni chochote tunachoona kuwa kitu bora zaidi ulimwenguni kwetu, kile tunachotafuta hasa maishani, kile tunachofikiri kingetupa furaha zaidi kuwa nacho, kile ambacho kitatupa huzuni zaidi kukosa. Inaweza kuwa ngono au umakini au nguvu au umaarufu au utajiri - kila moja ya malengo haya hufichua ukaidi wa Mungu mioyoni mwetu. Kwa hiyo, Baxter anaeleza, “sehemu kuu ya uharibifu wa mwanadamu katika hali yake ya asili potovu, hujumuisha wema mkuu mbaya, hazina mbaya, usalama usiofaa.”


Hakuna swali la uchunguzi linaloingia ndani kwa kina zaidi ndani yetu kama: Ni kitu gani kimoja ambacho siwezi kuishi pasipo kuwa nacho?


Katika mizizi, dhambi sio kufanya mabaya, ni kuabudu vibaya. Dhambi hushawishi mioyo yetu juu ya hazina yoyote au usalama unaochukua nafasi ya hazina na usalama tunaopata kwa Mungu pekee.


Sanamu

Kwa sababu sisi sote tunamkana Mungu katika mzizi (vipofu kwa furaha tele iliyopo kwa Mungu), macho yetu yanaongozwa kwa urahisi kutoka kwa sanamu moja hadi nyingine katika kukimbilia uzinzi wa kiroho. John Calvin anaeleza, “Wazinzi kwa mtazamo wao wa kutangatanga, huzalisha miali ya tamaa, na hivyo mioyo yao huwashwa moto”(Ezekieli 6:9). Hivyo ndivyo moyo unavyofanya kazi. Kwa kumpuuza Mungu asiyeonekana, tunaweka macho yetu kwenye kutafuta chochote tunachokiona katika ulimwengu huu unaoonekana. Tunachokiona karibu nasi, tunakiwinda, na kile tunachowinda huchochea zaidi tamaa ndani ya mioyo yetu kwa kile tunachokiona.


Hii inaeleza kwa nini sanamu huchukua mionekano tofauti tofauti katika kila karne au utamaduni. Wakati fulani sanamu ni mti unaochongwa kuwa mjusi, dhahabu iliyofinyangwa kuwa ndama, pembe za tembo zilizofanyizwa kuwa sanamu ya nyumbani, au jalada la gazeti lililochapishwa picha ya mwanamitindo. Kama vile mpanda miamba, macho yetu yanatazama huku na huku ili kupata kishikio kinachofuata, kila mshiko mpya ukichochea zaidi tamaa iliyo moyoni mwetu na kutusukuma kuelekea kilele cha utoshelevu usio na Mungu tunachofuata, lakini hilo halitapatikana kamwe.


Kupanda ni kazi bure kwa sababu mwisho haufiki kamwe. Lengo halikuwa sahihi tangu mwanzo - ulikuwa mlima usio sahihi. Na wakati wote, kwa kila hatua, tunaongeza tu urefu ambao hatimaye tutaanguka.


Hapa tunapata mzunguko usioisha wa dhambi. Hatimaye ni umauti na upofu, kutafuta raha za kidunia ambazo zinageuka kuwa kazi bure na kusababisha kukata tamaa zaidi katika kutafuta ahadi mpya za utimilifu katika aina mpya za kujieleza kwa ngono au kwa pesa zaidi au katika vifaa vipya zaidi.


Upotofu kamili


"Ikiwa nitaepukana na upotevu wangu, Mungu lazima awe hazina yangu kuu."

Huku kutafuta tafuta kwa nafsi iliyokufa kwa ajili ya kuridhika na utoshelevu katika anasa za mwili, ambapo raha ya kudumu haiwezi kupatikana, ndicho ambacho wafuasi wa Calvin wanakiita upotovu kamili,  herufi ya kwanza katika kifupi TULIP. Ufafanuzi huu ulitambuliwa katika Maandiko na Calvin mwenyewe na wengi hapo awali, na tangu katika Wapuritani, Waprincetoni, na Wakalvini leo. Kama John Piper asemavyo, “Upotovu kamili si ubaya tu, bali ni upofu wa kuona uzuri na kufa kwa furaha.”


Sisi sote hatujapangiwa kuwa Adolf Hitler, kuwa wakandamizaji. Kwa wengi wetu, uwezo wetu ni mdogo sana kulisha starehe za ubinafsi tunazoweza kufinya kutoka kwa taifa. Kiwango cha jinsi upotovu unavyoonyeshwa hutofautiana kwa sisi sote. Mara nyingi, upotovu huu katika mapenzi husababisha zaidi mawazo na ndoto zisizo na mpangilio kuliko tabia halisi. Kiwango cha uharibifu kinatofautiana, lakini mioyo yetu ni sawa.


Ni jambo moja kuwa mbaya; ni jambo lingine kabisa kuwa kipofu kwa wema. Sote tunapata uzoefu huu. Hiki ndicho kiini cha upotovu kamili - ndicho kinachofanya upotovu kuwa jumla kabisa - hatuwezi kuanza kufikiria jinsi gani hisia yoyote ya kweli ya furaha au starehe inaweza kupatikana kwa Mungu!


Tena, kurudi kwa Wapuritani wa zamani, ambao walielewa jinsi upotovu unavyofanya kazi. Walisema ni kuwa na mapenzi ya moyo ambayo "yamechochewa" - njia isiyo ya kawaida ya kusema mapenzi yameharibiwa kabisa. Upotovu unaharibu kile ambacho moyo uliumbwa kuwa na kufanya. Ni mtu mwenye kiu akinywa maji ya chumvi. Moyo wa asili hutamani tu kile ambacho humvunjia Mungu heshima na hatimaye hujiangamiza wenyewe.


Huzuni kubwa zaidi ya mtenda-dhambi ni kwamba “hawezi kuitosheleza tamaa yake mbaya, au kuridhisha mapenzi yake ya kimwili.” Wakati ulimwengu wa asili hauwezi kutoa raha zaidi, zisizo za asili husakwa (Warumi 1:18–32). Tamaa zake hazishibi, na tamaa zake za dhambi hazitosheki.

Kwa hivyo, ukweli wa upotovu kamili unatufikisha hapa. Tunapenda kile kinachotuangamiza; sisi ni vipofu kwa yale yanayoturidhisha. Upotovu kamili ni uharibifu kamili wa mapenzi ya roho. Ni upofu kamili wa uzuri wa Mungu. Ni upinzani kamili wa furaha katika Mungu. Ni asili ya dhambi zote.


Raha za Hatia

Janga la kweli ni kwamba yote ni suala la upendeleo. “Wanaume hupendelea peremende za kimwili kabla ya ushirika na Mungu,” aandika William Bates kuhusu upotovu. Kuzungumza truffles [uyoga wa thamani] sio jambo dogo. Kuwa mpotovu kabisa si kuwa muathirika asiye na hatia wa dhambi. Na si tu kumsahau Mungu, tatizo linaloweza kutatuliwa na kengele za iPhone au mahudhurio ya kila wiki kanisa. Upotovu ni wa hiari na wa makusudi na uasi wa kumpotezea Mungu, na kwa hivyo kunahitaji hukumu ya Mungu. Kufurahia anasa za mwili juu ya anasa za Mungu ni "dhambi ya hatia ya kushangaza, na ni chukizo kwa Mungu, na laana katika asili yake."


Kushikilia anasa za mwili "ni kifo"(Warumi 8: 6). Na kuna dawa moja tu ya upotovu huu usio na matumaini. Badala ya kufuata miongozo ya asili ya miili yetu, lazima tufuate ahadi ya furaha ya milele katika ushirika na Mungu ( Waebrania 11:24–26 ). Dhambi ni furaha iliyotiwa sumu. Utakatifu ni furaha iliyoahirishwa na kufuatwa. Ikiwa nitaepuka upotevu wangu, Mungu lazima awe hazina yangu kuu.


Inakuaje sasa?


“Wakalvinisti wa karne nyingi zilizopita wanajua, ili kupata furaha, ni lazima mtu aupige moyo wangu na kuvuruga mapenzi yangu.”

Hapo ndipo hadithi itakapoishia. Kwa sasa, ni lazima tutambue kuwa kumkana Mungu ni mchanga wa kuzama. Sisi sote lazima tuwe na furaha. Na kwa wenye dhambi, tunachagua dhambi badala ya Mungu. Upotovu kamili ni kuwa na hii hali ya kutokuweza kujisaidia kabisa..


Na bado, “Bwana hasemi kuhusu dhambi yako ili ufikiri kwamba wewe ni takataka,” aandika Mkalvini mmoja wa siku hizi. "Anazungumza juu yake kwa sababu tu wewe sio takataka. Anazungumza juu yake kwa sababu alikuumba kwa mfano wake mwenyewe, na mpango wa juu zaidi na mzuri zaidi kwako kuliko ule uliojichagulia.


Hapa ndipo hadithi hupinduka. Mungu hufunua upotovu ili kuvunja wale anaowaongoza kuelekea furaha ya kweli. Lakini kwa kuzingatia janga la kibinadamu linaloitwa upotovu kamili, mpango mkali kama huo unaonekana kuwa hauwezekani mbali na aina fulani ya ukiukwaji wa kimungu wa ujasiri juu ya shughuli zangu. Iwapo nitaishi, ni lazima kitu au mtu anizuie. Lazima mtu anivunje.


Wakalvini kwa karne nyingi zilizopita walijua, ili kupata furaha, ni lazima mtu aupige moyo wangu na kuvuruga mapenzi yangu. Mtu lazima aondoe macho yangu kutoka kwa sanamu na kunifunika kwa uzuri zaidi.

 

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page