top of page

Mtazamo wa Furaha Kamilifu ya Kikristo: Wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi

  • Writer: Dalvin Mwamakula
    Dalvin Mwamakula
  • Apr 3
  • 4 min read
ree

ree

Makala imeandwika na John Piper

Mwanzilishi na Mwalimu, desiringGod.org


Kutetea mtazamo wa furaha kamilifu ya Kikristo - yaani Mtazamo wa Hedonismi ya Kikristo kiufafanuzi ni jambo moja; lakini kusaidia watu kuhisi maadili yake ni kitu kingine. Jambo la mwisho ni gumu zaidi kulifanya. Hicho ndicho ninachotaka kujaribu kufanya hapa.


Lakini kwanza, kitu hiki ni nini?


Mtazamo wa furaha kamilifu ya Kikristo, ni njia ya maisha iliyojikita mizizi yake katika imani kwamba Mungu hutukuzwa zaidi ndani yetu tunaporidhika zaidi ndani yake. Matawi na matunda ya mzizi huu yanajumuisha yote na yanasisimua. Yanahusisha dokezo lenye kustaajabisha ya kwamba wema wote wa kweli, na ibada yote ya kweli, lazima ijumuishe kutafuta furaha katika Mungu.


Sababu ya hili ni kwamba wema wote wa kweli na ibada yote ya kweli lazima ihusishe nia ya kumtukuza Mungu. Hii ni kwa sababu tuliumbwa ili tumtukuze Mungu (Isaya 43:7), na kwa sababu Paulo alisema, “Lolote mfanyalo, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” (1 Wakorintho 10:31). Kwa hiyo ni dhambi kufuata wema wowote, au ibada yoyote, bila nia ya kumtukuza Mungu.


Lakini Mungu hatukuzwi pale tunapomwona hapendezi zaidi kuliko vitu vingine. Anadharauliwa. Kwa kujua hili, hatuwezi kuwa wazembe kuhusu iwapo tunampendeza Mungu katika matendo tunayoyafuatilia. Katika matendo hayo yote, ikiwa tunataka kumtukuza Mungu, ni lazima tuwe na lengo la kumuona anayependeza zaidi kuliko kitu kingine chochote.


Yesu aliposema, “Ni heri kutoa kuliko kupokea” (Matendo 20:35), hakumaanisha kwamba tunapaswa kupuuza ukweli huu tunapotoa. Kwa kweli, Paulo alisema, katika andiko hilohilo, tunapaswa “kulikumbuka” tunapotoa. Tamaa ya kubarikiwa kupitia kutoa kwa wengine huwa ya ubinafsi na ya kimaslahi iwapo baraka tunayoitamani si Mungu mwenyewe, na haikusudii kuwachukua wengine pamoja nasi kuingia katika furaha hii kupitia matoleo yetu.


Mtazamo wa furaha kamilifu ya Kikristo ni njia ya maisha inayoamini kwamba: "Mungu hutukuzwa zaidi ndani yetu tunaporidhika zaidi ndani yake."

Kuelewa Usemi Unaopendwa

Lakini yote hayo hayafikii kikamilifu dhamira — hisia, roho, mwelekeo, na mtindo — wa mtazamo wa furaha kamilifu ya Kikristo. Maneno ya kibiblia ambayo tumetumia zaidi ya mengine kuelezea ukweli huu yamechukuliwa kutoka 2 Wakorintho 6:10: "tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi;"


Ni mara chache sana nichambua kifungu hiki kwa kina kulingana na maana yake ya maandiko, au kutoa mifano ya kueleweka. Hivi sasa, nataka kufanya yote mawili kwa ufupi.


Katika 2 Wakorintho 6:3–10, Paulo anaonyesha jinsi anavyojitahidi kutowekwa kikwazo chochote kwa mtu yeyote kupitia mtindo wake wa maisha (kifungu cha 3), bali anajidhihirisha kuwa mtumishi wa kweli kwa kila njia awezayo — kwa kupitia aina thelathini za hali na matukio tofauti!


Miongoni mwa hali hizo thelathini ni “mwenye huzuni, lakini akifurahi siku zote.” Inatokea kati ya jozi kadhaa zinazofanana:


“tukiwa kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli; tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi; tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.” (2 Wakorintho 6:8–10).


Kilicho Kweli Kuhusu Paulo

Wakati mmoja niliulizwa kwa nini nachukulia “kuhuzunika” kama jambo la kweli kuhusu Paulo, ilhali mengine katika orodha hii yana kitu cha uongo ambacho baadaye kinasahihishwa. Kama: ". . . kama wadanganyifu, na bado ni wa kweli”? Labda Paulo anamaanisha anatazamwa kama "huzuni" lakini sivyo, bali anafurahi daima.


Sababu ya kutofikiri hivyo ndivyo Paulo anamaanisha ni kwamba Paulo anahama kutoka kwa jozi zinazotofautisha uwongo na kweli (kama “kama wadanganyifu, lakini wa kweli”), na kwenda kwa jozi ambazo zote mbili ni za kweli (kama “kama maskini, lakini huwatajirisha wengi”).


Katika njia ya Paulo ya kufikiri, “kutojulikana,” “kufa,” “nidhamu,” “huzuni,” “maskini,” na “kutokuwa na kitu,” yote ni kweli kwake. Kwa hiyo mwanzoni mwa mstari wa 9, alihama kutoka kwa madai ya uwongo yaliyosahihishwa na yale ya kweli, na akaanza kuorodhesha jozi ambazo zote mbili ni za kweli, lakini zenye utata: kutojulikana/maarufu, wanaokufa/hai, wenye kuadhibiwa/hawaku-uawa, wenye huzuni/furaha, maskini/ wenye kutajirisha.


Kwa hiyo ndiyo, Paulo anajiona kuwa kweli “mwenye huzuni.” Jambo ambalo si la kushangaza kwa kuzingatia Warumi 9:2: “Nina huzuni kuu na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. . . kwa ajili ya ndugu zangu wa taifa langu kwa jinsi ya mwili.” Huzuni na maumivu yasiyokoma. Inashangaza!

Ikiwa hii ilikuwa kweli kwa mtume mkuu wa furaha, ni zaidi kiasi gani kwetu. Hakika maisha yetu yatakuwa na majonzi ya kudumu (na furaha) pia. Ikiwa maisha yetu hayahuzunishwi, inaweza kuwa kwamba hatuwapendi waliopotea jinsi Paulo alivyowapenda.


Aina Nzito ya Furaha

Kwa hiyo, maadili ya furaha ya Kikristo si furaha au shangwe iliyo nyepesi, isiyo makini, ya mzaha, isiyo na uzito, ya juujuu, ya kipuuzi, au ya ucheshi. Hii inamaanisha kwamba kuna sehemu kubwa ya jinsi baadhi ya watu wanafanya ibada kanisani ambayo ni ngeni kwa Hedonismi ya Kikristo. Furaha ya mtazamo wa furaha ya Kikristo sio ya kuchekesha. Mtazamo wa furaha ya Kikristo inaweza kushikwa kabisa na kicheko, lakini hili halihusiani sana na hali ya wepesi wa moyo isiyo na nafasi kwa furaha ya kina na ya uzito.


CS Lewis alisema, “Joy is the serious business of heaven” (Letters to Malcolm, 1964, 299). Amina. Naye akasema, “Lazima tucheze. Lakini furaha yetu lazima iwe ya aina hiyo (na kwa kweli, ni aina ya furaha zaidi) ambayo ipo kati ya watu ambao, tangu awali, wamechukuliana kwa uzito — hakuna kukurupuka, hakuna ubora, hakuna kudhaniwa" (Christian Reflections, 1967, 10).


Kuna moyo mwororo ambao hufurahi pamoja na wale wanaofurahi na kulia na wale wanaolia — wakati huo huo. Wakati mwingine kimoja kinaonekana zaidi. Wakati mwingine kingine. Lakini kila moja huathiri na kuimarisha ladha ya nyingine.. Unaweza kuonja ladha ya kipekee ya furaha hii na huzuni hii.


Hapa kuna kielelezo kimoja cha kufunga cha jinsi inavyoonekana — inavyohisika. Hii inatoka kwenye Religious Affections ya Jonathan Edwards. Huyu ndiye Mkristo mwenye mtazamo wa furaha kamilifu ya kikristo, katika ubora wake.


Kadri anavyokuwa na ujasiri mtakatifu zaidi, ndivyo anavyokuwa na kujitumainisha kidogo ndani ya nafsi yake… na unyenyekevu mwingi zaidi. Kadri anavyokuwa na uhakika zaidi kuliko wengine wa ukombozi kutoka kuzimu, ndivyo anavyohisi zaidi kuwa anastahili adhabu yake. Yeye hana uwezekano mkubwa kama wengine wa kutikiswa katika imani, lakini ana uwezekano mkubwa zaidi wa kuguswa na maonyo mazito, na hasira ya Mungu, na maafa ya wengine. Ana faraja iliyo thabiti zaidi, lakini moyo ulio mpole zaidi: tajiri kuliko wengine, lakini maskini zaidi ya wote kwa roho; mtakatifu aliye mrefu na mwenye nguvu zaidi, lakini mtoto mdogo na mwororo zaidi kati yao. (Works, Vol. 2, Yale, 364) 

 

 

Comments


100Fold Logo

NJIA ZA KUTUFUATILIA

  • Youtube
  • WhatsApp
  • Email
  • Facebook
  • Instagram
bottom of page