top of page



"Maneno yako ni matamu kama nini kwangu, Ni matamu kuliko asali kinywani mwangu!"

"Furaha ya Mungu katika Mwana wake itakuwa ndani yetu na itakuwa yetu - furaha yetu katika Mwana. Na hili halitaisha, kwa sababu Baba wala Mwana hawana mwisho."

"Mungu anapenda kuonyesha uungu wake kwa kunifanyia kazi, na kazi yake kwangu daima ni kabla na chini, ndani, na katika kazi yoyote ninayofanya kwa ajili yake."

"Mwili wa nani? wa Kristo. Dhambi ya nani ilihukumiwa katika mwili huo? Zetu. Kwetu sisi basi? Hakuna hukumu! "

"Kwasababu kiini cha utukufu wake ni utimilifu wa neema inayofurika katika wema kwa wahitaji."

"Wivu wa Mungu ni tishio kwa wanaofanya ukahaba na kuiuza mioyo yao kwa ulimwengu, lakini ni faraja kwa wanaoshika nadhiri za agano na kuwa wageni duniani."

"Ubinafsi unatafuta furaha ya kibinafsi kwa gharama ya wengine. Upendo kama wa Kristo unatafuta furaha yake katika furaha ya wengine - si kwa gharama zao."

"Wake, tafuteni furaha yenu kwa kuthibitisha na kuwaheshimu waume zenu kama viongozi. Waume, tafuteni furaha yenu kwa kuwaongoza na kujitoa kwa wake zenu kama Kristo alivyofanya kwa kanisa."

"Neema kuu ya Mungu, inayofanya yasiyowezekana kwa wanadamu, kupitia injili ya Yesu Kristo, ndiyo tumaini kuu la kimishonari."

"Kwa wamisionari watarajiwa, Yesu anasema, “Naahidi kufanya kazi kwa ajili yenu, na kuwa kwa ajili yenu, kiasi kwamba hamtaweza kusema kuwa mmetoa dhabihu yoyote.”"

"Kila hatua muhimu niliyowahi kuchukua katika kuelewa kina cha upendo wa Mungu na kukua kwa undani naye imekuja kupitia mateso."

"Mungu hatosheki kamwe kutupa ulinzi wa moto wake; analenga kutupa raha ya uwepo wake. Ninazipenda "Nita" za Mungu!"

"Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, dhiki, au shida, au mateso, au njaa, au utupu, au hatari, au upanga?"

"Je, si upumbavu kukubali mkataba wa neema kisha kupanga njia ya kuilipia? Neema inapaswa kuwa bure, hivyo hatuwezi kuichukulia kama kitu kinachohitaji kulipiwa."

"Wasiwasi haufanyi chochote cha maana. Hiyo ni ahadi. Iamini. Itendee kazi."

"Furaha ya kuwa na Yesu ni mstari usiokatika kutoka sasa hadi umilele. Hautokatwa - si kwa kifo chake au chetu."

"Ili tuwe huru kabisa, ni lazima tuwe na shauku, uwezo, na fursa ya kufanya mambo ambayo yatatufanya tuwe na furaha milele. Bila majuto."

"Msijisumbue juu ya kitu chochote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu zijulikane na Mungu."

"Kazi kubwa ya upendo ilifanikishwa kwa sababu Yesu alitafuta furaha kuu zaidi: kutukuzwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu katika kusanyiko la waliokombolewa."

"Ahadi za neema ya Mungu zinatoa nguvu zinazofanya matakwa ya utakatifu wa Mungu kuwa uzoefu wa uhuru badala ya hofu na kifungo."

"Sifa ya kweli inamaanisha furaha kamili, na kusudi la juu kabisa la mwanadamu ni kunywa kwa kina katika furaha hii kwa ajili ya utukufu wa Mungu."

“Tuombe pamoja kwamba Mungu wetu mkuu asiye na mwisho aelekeze mioyo yetu kwake, na afungue macho yetu ili tumwone kadiri tuwezavyo, na tuwe na shauku ya kumjua zaidi.”

“Tunaweza kuwa na uhakika kwamba makosa yote yatashughulikiwa na Mungu na kwamba tunaweza kuyaacha mikononi mwake kwa sababu kisasi ni cha Bwana.”

“Imani inayookoa ni kutambua uchukizo wa dhambi, utakatifu wa Mungu, na uzuri wa msamaha wake, na kutamani urafiki mpya na Mungu mwenye kusamehe.”

“Kwa hiyo, Roho alikuja mara ya kwanza, na Roho anaendelea kusambazwa, kwa njia ya imani. Chochote anachofanya ndani na kupitia kwetu ni kwa imani.”

“Huduma ni mtindo wa maisha unaojitoa kwa Kristo na kukidhi mahitaji ya wengine, ikifanywa na Wakristo wa kawaida waliotayarishwa na Wachungaji wao.”

“Kuna neema ya ajabu
Ya siku zijazo ya kutarajiwa
wakati wa uhitaji. Kila tendo jipya la nguvu linashuhudia neema isiyobadilika inayotolewa kila wakati.”

“Imani haitosheki na “anasa za haraka.” Ina njaa kubwa kwa ajili ya furaha. Furaha inayodumu. Milele.”

“Moyo unaopenda pesa—hutegemea pesa kwa ajili ya furaha—hautegemei utoshelevu wa Mungu ndani ya Yesu.”

“Kifo cha mashahidi sio jambo la bahati mbaya. Haikumshangaza Mungu. Si kitu kisichotarajiwa.”

"Lengo letu ni kutumainia upendo wake thabiti. Kumkimbilia. Kumfurahia Mungu, kumthamini na kufurahia ushirika na kibali chake."

"Hii ni njia ya kumpa kisasi Yeye ambaye kinamhusu. Kisasi ni changu, asema Bwana. Unakiweka chini. Nitakichukua. Haki itatendeka."

"Kwa Mungu, sifa ni mwangwi mzuri wa ubora wake katika mioyo ya watu wake.
Kwetu sisi, sifa ni kilele cha kuridhika kinachotokana na kuishi katika ushirika na Mungu."

"Tunamwomba Mungu atufanyie sisi kwa njia ya Kristo yale ambayo hatuwezi kujifanyia wenyewe—kuzaa matunda."

"Mungu atawaponya kwa kuwanyenyekeza. Atamponya mgonjwa kwa kukiponda kiburi chake."

"Viwanda vikubwa na mishahara mikubwa ni ukweli wa nyakati zetu, na si lazima iwe mbaya. Ubaya ni kudhani mshahara mkubwa lazima uambatane na maisha ya kifahari."

"Mungu anatuita tusikie Neno lake la mwisho, la uamuzi, lisilokoma — kulitafakari, kulisoma, kulihifadhi akilini, kulikawia, na kulifikiria hadi litujaze kabisa ndani ya nafsi zetu."

"“Mambo yote yanawezekana kwa Mungu!” — mbele maneno hayo yanatoa tumaini, na nyuma yanatoa unyenyekevu. Hayo ni tiba ya kukata tamaa na tiba ya kiburi — dawa kamili ya wamishonari."

"Hivyo, mateso yote yanayokuja katika njia ya utii ni mateso pamoja na Kristo na kwa ajili ya Kristo — iwe ni saratani ukiwa nyumbani au kuteswa ukiwa mbali."

"Mungu kamwe hawi mwathirika wa hali. Yeye halazimishwi kamwe katika hali ya kulazimishwa kufanya kitu ambacho hawezi kukifurahia. Yeye hadhihakiwi. Yeye habanwi, hapingwi wala kulazimishwa."

"Tofauti kuu ni kwamba:
(1) Masihi, Yesu, amekuja na kumwaga damu ya agano jipya kwa wokovu wa wote;
(2) agano la kale haliwatawali watu wa agano jipya la Mungu; na
(3) moyo mpya na nguvu ya Roho Mtakatifu imetolewa kwa njia ya imani."

"Kwa hiyo mantiki ya kutoogopa katika uso wa dhiki ni ukweli huu maradufu: Shida yako na imani yako katika uso wa dhiki ni zawadi za Mungu."

"Tunapambana na mahangaiko kwa kupigana na kutokuamini na kupigania imani katika neema ya wakati ujao."

"Kila siku ina shida zake. Lakini kamwe si zaidi ya unavyoweza kustahimili kwa neema Yake."

"Furaha yetu haiinuki tu kutoka katika mtazamo wa kipindi cha nyuma kwa shukrani. Huinuka pia kutoka katika mtazamo wa mbele kwa matumaini"

"Katika Yesu Kristo sisi tuliozaliwa na Mungu tunayo fursa isiyoelezeka ya kumjua Yehova kama Baba yetu - MIMI NIKO AMBAYE NIKO - Mungu."

"Je, tujikane wenyewe na kuwapenda wengine kama Mungu anavyotupenda sisi na kuhatarisha mali na maisha yetu? Au tubaki "salama" ?"

"Maisha yetu ya kimwili yanaumbwa na kudumisha na neno la Mungu, na maisha yetu ya kiroho yanahuishwa na kudumishwa na neno la Mungu."

"Nia ya Mungu ni kukuza utimilifu wa utukufu wake kwa kumwaga rehema kwetu - kwetu sisi wenye dhambi, ambao tunamhitaji sana."

“Kristo alishinda uchungu na kisasi kwa imani katika ahadi za Mungu, Hakimu mwema. Je, sisi tunapaswa kufanya nini zaidi, kwa kuwa tuna haki ndogo ya kunung'unika kwa kuteswa kuliko yeye?”

“Biblia inatupa mtazamo wa kustaajabisha katika nafsi ya Yesu usiku kabla ya kusulubiwa kwake. Tazama na ujifunze kutokana na jinsi Yesu alivyopigana vita vyake vya kimkakati dhidi ya kukata tamaa au sonona.”

“Lakini imani katika neema ya wakati ujao huzaa upendo kwa kuondoa hatia na hofu na uchoyo kutoka moyoni.”

“Neema ndiye mwamuzi mkuu katika huduma ya Paulo, ikimpa nguvu ya kutekeleza kazi yake.”

“Kusudi la karama za kiroho ni kupokea na kusambaza neema ya Mungu ya wakati ujao kwa mahitaji hayo.”

““Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.” Tunajihubiria hivyo. Na tunaitupa kwenye uso wa Shetani. Na tunaiamini.”

“Kwa hivyo, kazi kuu ya Shetani ni kutetea, kukuza, kusaidia, kutisha, na kuthibitisha mwelekeo wetu wa kutenda dhambi. Na kutuonda katika imani na kutuzuia kutubu.”

“Majanga yote makubwa duniani yanaweza kuua mwili tu. Lakini tusipopigana na tamaa, tunapoteza nafsi zetu. Milele.”

“Kusudi moja yapo la kutikiswa na kuteseka ni kufanya imani zetu zisitikisike zaidi.”

"Mungu hatuhitaji sisi, bali kujitosheleza kwake kusiko na kikomo kumemwagika kwa upendo kwetu wenye dhambi tunaomhitaji yeye, na zawadi ya nafsi yake katika Yesu"

"Ikiwa Mungu hana furaha, basi lengo la injili si lengo la furaha, na hiyo inamaanisha kuwa isingekuwa injili hata kidogo."

"Kifo cha Kristo ni hekima ya Mungu kwamba upendo wa Mungu huwaokoa wenye dhambi kutoka katika ghadhabu ya Mungu, huku ukishikilia na kudhihirisha haki ya Mungu katika Kristo."

"Hatumtukuzi Mungu kwa kumhudumia mahitaji yake, bali kwa kuomba atutimizie yetu, kutumaini atajibu, na kuishi kwa furaha tunakijitoa kwa upendo kwa wengine."

"Hatuombi si kwasababu hatutaki kuomba. Hatuombi kwasababu hatupangi kuomba. Matokeo ya kutokupanga kuomba ni kurudia yale yale ya zamani."

"Unapompenda mtu ambaye Mungu amekufanya kuwa mwili mmoja, unajipenda mwenyewe. Yaani furaha yako kuu inapatikana katika kutafuta furaha kuu ya mwenzi wako."

"Alipanga ndoa kwa makusudi sana ifanane na uhusiano kati ya Mwanawe na kanisa, ambao alikuwa ameupanga tangu milele."

"Yesu uhusiana na mungu namna ambavyo miali au mng'ao uhusiana na utukufu, au namna ambavyo miali ya mwanga wa jua uhusiana na jua."

"Kama furaha yako ni kupata neema ya Mungu inayokujaza na kumwagika kwa manufaa ya wengine, Mungu atafanya yasiyowezekana kupitia wewe kwa ajili ya wokovu wa watu ambao hawajafikiwa."

"Maisha ya dunia hii si ziwa, ni mto unaotiririka kuelekea uharibifu. Usipomsikiliza Yesu kwa bidii na kumtazama kila saa, hutosimama ulipo, utarudi nyuma na kuelea mbali na Kristo."

"Ni uhuru wa kushangaza na kutokuwa na masharti kwa neema ya uteuzi — ikifuatiwa na kazi zote nyingine za neema ya wokovu — vinavyoturuhusu kuchukua na kuonja zawadi hizo kama zetu wenyewe bila kujikweza."

"Je, furaha kuu zaidi inayomtukuza Kristo haipatikani kwa kumtazama Yesu siku nzima na kupaza sauti, “Wewe ni wa ajabu!” “Wewe ni wa ajabu!""

"Kumlipa Bwana ni kuendelea kupokea kutoka kwake ili wema wake utukuzwe. Kuinua kikombe cha wokovu kunamaanisha kuunywa wokovu wa Bwana huku ukitarajia zaidi."

"Zaidi ya hayo, haijalishi nini kitatokea, Mungu atafufua mwili wako siku moja na kuhifadhi maisha na mwili wako kwa ushirika wake wa milele."

"Tunapaswa kupigana na kutokuamini kwa wasiwasi kwa kutumia ahadi za neema ya wakati ujao."

Ninamshukuru Mungu kwamba tena na tena ameuamsha moyo wangu kumtamani, kumwona, na kuketi kwenye karamu ya Furaha ya Kikristo na kumwabudu Mfalme wa Utukufu."

"Kujitolea maisha kwa starehe za kimwili, usalama, na msisimko ni kama kutupa pesa kwenye shimo la panya."

"Ina maana kwamba inapokuja suala la kuwa mtarajiwa wa neema, historia yako haina uhusiano wowote na chaguo la Mungu. Hiyo ni habari njema."

"Geuka kutoka dhambini na umtumaini Bwana Yesu Kristo; na uweza wa Mungu Mwenyezi utakuwa heshima ya roho yako, malipo ya maadui zako, na kimbilio la maisha yako — milele."

"Kutokuamini ahadi za Mungu ni mzizi wa wasiwasi, ambao, kwa upande wake, ni mzizi wa dhambi nyingine nyingi."

"Nimefanya jina lako lijulikane kwao nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”

“Mateso ya Kristo yalikuwa malipo ya Mungu kwa maumivu yote uliopata kutoka kwa Mkristo mwenzako. Ukristo haupunguzi uzito wa dhambi wala hauongezi matusi kwa majeraha yetu.”

“Moyo wa imani ni tofauti kabisa. Tamaa zake zinaendelea kuwa kali ukitazamia siku zijazo. Lakini, kile Unachotamani ni kuridhika kikamilifu kwa kupata yote ambayo Mungu ni kwa ajili yetu kupitia Yesu.”

“Nguvu tunazohitaji sasa
na katika miongo ijayo zinatoka kwa Kristo mwenye nguvu, ambaye daima yupo kutenda kwa ajili ya mapenzi yake mema.”

“Maombi ni aina ya imani inayotuunganisha leo na neema ambayo itatufanya tuwe na uwezo wa huduma ya kesho. Kuzigatia muda ni muhimu sana.”

“Vita dhidi ya kukata tamaa ni vita ya kuamini ahadi za Mungu. Na imani hiyo katika neema ya Mungu ya wakati ujao inakuja kwa kusikia neno. Na hivyo kujihubiria neno la Mungu ni kiini cha vita.”

“Kwa hivyo, kazi kuu ya Shetani ni kutetea, kukuza, kusaidia, kutisha, na kuthibitisha mwelekeo wetu wa kutenda dhambi. Na kutuonda katika imani na kutuzuia kutubu.”

“Ukidhani mateso yako hayana maana, utajitenga na Mungu. Ni muhimu kuamini kwamba Mungu hutoa neema kupitia mateso.”
bottom of page

























































































































































































































